Skip to main content

NGURUWE 612 WAFA KWA MAFUA LUDEWA DC APIGA MARUFUKU WATU KUMLA MNYAMA HUYO


LUDEWA
MKUU wa Wilaya ya Ludewa Bi. Georgina Bundala amepiga marufuku kwa muda usiojulikana kuchinja au kula na kusafirisha nguruwe pamoja na mazao yake kama vile nyama, mifupa, nywele na mazao ya kusindika kutokana na homa ya nguruwe kupiga hodi tena wilayani humo.
Bi. Bundala alisema endapo mfanyabiashara au mfugaji yeyote atabainika akisafirisha nguruwe kutoka katika maeneo yaliyoathirika na kupeleka maeneo yasiyoathirika mtu huyo atakuwa amekiuka agizo na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha amewaagiza wataalamu wote wa kilimo na mifugo, maafisa watendaji kata na vijiji kusimamia agizo hili ili kuwathibiti wale wote wasiokuwa waaminifu wanaosafirisha nyama ya nguruwe kwa siri wakidhani wanajificha.
Akitoa taarifa na takwimu za ugonjwa huo kwa Mkuu wa Wilaya, Daktari wa Mifugo wilayani Ludewa Bw. Festo Mkomba alisema maambukizi mapya ya homa ya nguruwe yametokea katika tarafa ya Mwambao wa Ziwa Nyasa na sasa yapo katika tarafa ya Mawengi.
Dr. Mkomba alisema tangu ugonjwa huo uingie wilayani Ludewa tayari nguruwe 612 kati ya nguruwe 2,356 waliopo wilayani humo wameshakufa na kwamba Lumbila wamekufa 154, Lupingu 214, Kilondo 148 na Mawengi 40 na kusema kasi hiyo ni kubwa sana kiuchumi.
Katika tangazo lake kwa wananchi Bw. Festo Mkomba ambaye ni Daktari wa mifugo wilayani Ludewa alisema kuanzia Septemba 20 mwaka huu Wilaya ya Ludewa itakuwa chini ya karantini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo kutokana na matukio ya homa ya nguruwe kujitokeza tena wilayani Ludewa.
Awali, Bw. Marco Mhagama mtaalamu wa mifugo alisema wafanyabiashara, wafugaji na walazi ndio wanaosababisha kurudiarudia kwa ugonjwa huo kwani wamekuwa na tabia ya kupuuzia maelekezo wanayopewa na wataalamu wa mifugo juu ya kukabiliana na homa ya nguruwe.
Bw. Mhagama alisema kuwa kimsingi na kitaalamu homa ya nguruwe haina madhara ya moja kwa moja katika afya ya binadamu, lakini wananchi wengi wilayani Ludewa wanategemea mifugo hiyo katika kuinua uchumi na kuongeza kipato chao.
“Februari mwaka huu katantini kama hiyo iliwekwa baada ya ugonjwa huo kuua idadi kubwa ya nguruwe na baadaye mwezi June tuliruhusu kuanza kuchinjwa na kula, lakini wananchi wenyewe wamekuwa wazembe kwa kukosa uaminifu,” alisema mhagama.
Homa ya mafua ya nguruwe siku zote imekuwa ikiingia wilayani Ludewa kupitia vijiji vilivyopo kandokando ya Ziwa Nyasa na kwamba asili ya  ugonjwa huo ni kutoka nchi jirani ya Malawi kupitia wafanyabiashara wa Kyela, hivyo kuna kila sababu ya serikali kuongeza nguvu ya ziada katika kuthibiti homa hii katika maeneo hayo. 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...