Skip to main content

ASKOFU MTEGA

Na Basil Makungu,
Ludewa  

IKIWA imetimia zaidi ya wiki moja tangu kuuawa kwa Rais wa zamani wa Libya Muamar Gadaffi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Norbert Mtega amewataka viongozi wa Afrika kujali na kuheshimu haki za raia wao kwani mwenye kuua kwa upanga hufa kwa upanga.
Askofu Mkuu Mtega aliyasema hayo jana katika Misa ya shukrani na sherehe yake ya kutimiza miaka 25 ya uaskofu iliyofanyika katika Parokia ya Yesu Kristo Mkombozi, lililoko mjini Ludewa mkoani Iringa.
Askofu Mtega alisema yeye anachukia sana viongozi wenye dhuruma kwa raia wake na kuwataka viongozi wa Afrika kuacha ubabe, kuacha unafiki na kwamba tukio la Libya liwe changamoto kwao na kuwataka waache kuendesha nchi kama asasi binafsi kwani wananchi wanapochoka kwao kila kitu ni silaha.
“Tazameni na oneni enyi viongozi wa Afrika jinsi kiongozi mwafrika ambaye amepewa nafasi na dhamana ya kuongoza wananchi anavyoweza kukosea na kupitiwa kwa ulevi wa madaraka huku anasema yeye anawapenda watu wake huku akiendelea kuwaua,”alihuzunika Baba Askofu.
Askofu Mtega aliwaambia viongozi wa Afrika kuwa kuongoza nchi ni dhamana wanayopewa na mwenyezi Mungu kupitia watu wao, ili uongoze watu lazima kwanza uwapende, uwaheshimu, utambue na kuthamini utu na haki za Binadamu na kuthamini kwa kugawana kwa usawa kile kilichopo bila upendeleo.
Alisema fursa sawa kwa wote ndiyo silaha kwa kiongozi, lakini anapoanza kupotoka na kujitazama yeye binafsi au familia yake na marafiki huku watu wa kawaida hasa masikini hawana kitu na ndiyo maana wanapokuwa wamechoka na kugundua haki zao hutumia umoja wao kama silaha. Mtega aliwataka viongozi wa Afrika kuwajibika katika kuongoza nchi zao kwa kuzikabili mapema kero za wananchi na mambo yote yanayochukiza na kuchokoza raia, wasingoje mpaka waje kujaa hasira na jazba kwani hatua hiyo hupelekea kutenda vitendo vya mauaji watambue wajibu zao zinatoka kwa Mungu.
Akizungumzia kifo cha Rais wa Libya aliyeondolewa madarakani kwa kuuawa na majeshi ya NATO Muamar Gadaffi, Askofu Mkuu Mtega alisema kuuawa kwake ni tukio litakalobadilisha historia ya wana Libya. Alisema tunasikitika kuuawa kinyama, lakini alikwisha pewa nafasi na fursa nyingi za kujisalimisha ili asiuawe, lakini alikaidi na kuendelea kung’ang’ania.
Ameua watu wengi sana wa Taifa lake bila ya hatia wala sababu yoyote ya msingi. Aidha, amewataka wanaLibya wakae chini kwanza wapoe, watulize hasira, jazba na chuki yao na kwamba kama walimchukia Gadaffi kwa mambo na vitendo vyake viovu, basi mambo hayo wasiyatende wala kuyaendeleza kwa kuua, kugombanisha, na kuchukia watu.
Alisema kama Wana Libya watakaa pamoja na kuunda Serikali ambayo itatazama suala la upatanishi, upendo, ushirikiano, na umoja wa kitaifa itakuwa na mwanzo mzuri kuliko kuanza kulipa visasi kwa wale wote waliokuwa wafuasi wa Gadaffi.
Aliongeza kuwa Libya inakabiliwa na changamoto nyingi sana kwa sababu Gadaffi tunafahamu kwa ujanja wake alikuwa na wafuasi wengi na hata marafiki wa nje na ndani ya nchi yake kwa hiyo ni matumaini yetu kuwa Serikali mpya itatambua umuhimu wa upatanisho hakuna njia nyingine zaidi ya kusahau ugomvi na chuki na sasa waanze kulijenga Taifa lao ambalo limebomolewa sana.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...