Skip to main content

UHABA WA HUDUMA YA AFYA YAWAKUMBA WANANCHI WA KIJIJI CHA MLANGALI


Na Friday Simbaya, Ludewa
Wananchi wa Kijiji cha Mlangali Kata ya Mlangali wilayani Ludewa, mkoani Iringa wameiomba serikali  iwafungulie zahanati yao waliyoijenga kwa nguvu zao wenyewe  ili waweze kupata huduma ya afya  jirani, kwa sasa wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta  matibabu katika Kituo  Cha Mlangali ambacho kipo zaidi ya kilometa nne.
Wakiongea na Nipashe jana Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlangali Bw. David Mtitu na Mtendaji wa Kijiji  (VEO) Bw. Leo Mlelwa kwa pamoja walisema kuwa wananchi wa kijiji hicho wanapata shida sana kupata huduma ya afya kutokana na kijiji chao kukosa  zahanati, wakati wana zahanati yao waliyoijenga kwa nguvu zao. Walisema kuwa zahanati yao hipo tayari ,lakini hadi sasa haijafunguliwa.
“Pamoja na kuitikia wito wa Serikali wa kutaka kila  kijiji kuwa na zahanati na sisi kama wanakijiji cha Mlangali tuliitikia wito huo na tukaamua kujenga zahanati yetu, lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba hadi sasa haijafungiliwa pamoja na kuwa  kila kitu kimekamilika, ikiwa ni pamoja na nyumba ya mganga,” walisema viongozi hao.
Walisema kuwa kila kitu kimekalika mpaka nyumba ya mganga na choo, lakini cha cha ajabu ni kwamba zahanati  bado haijazinduliwa kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwa mwanachi wa kijiji cha Mlangali, ili kuwapunguzia wananchi adha ya kutembea mwendo mrefu kutafuta matibabu.
“Tuna mengi ya kuzungumza, lakini kwa leo ngoja tuseme haya machache tu….. kuna kipindi tunapata shida kuwasafirisha wagonjwa wetu hadi Kituo cha afya Mlangali ambacho kipo umbali wa kilometa zaidi ya nne (4km), na pengine kabla ya kufika kituo cha afya chenyewe mgonjwa anafia njiani. Kumbe kungekuwepo na zahanati jirani matatizo kama haya yanapungua, ndiyo maana tunaomba serikali yetu iharakishe kutufungulia zahanati yetu kwa sababu kila kitu kipo tayari mpaka nyumba ya mganga pamoja na choo,” walisema viongozi hao.
Zahanati ya Mlangali iliyopo Kijiji cha Mlangali ilianza rasmi kujengwa  mwaka  2008 na kukamilika  mwaka 2010 kwa gharama ya shilingi 19,194,000/-, ambapo nguvu za wananchi zilikuwa ni shilingi 14,140,000/-, Halmashauri ya Ludewa ilichangia shilingi 3,800,000/- na pesa ya wahisani ni shilingi 1,254,000/-.
Kijiji cha Mlangali ni moja ya vijiji saba vya Kata ya Mlangali ambacho kina wakazi  zaidi ya 2,360, vijijii  vingine katika kata hiyo ni pamoja na Itunda, Lufunbu, Ligumbilo, Masimbwe, Mkiu na Kiyombo. Kijiji cha Mlangali kina shule mbili tu ambazo ni Shule ya Msingi ya Itunda na Shule ya Sekondari ya Ulayasi.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ludewa (DMO), Dkt. Happiness Ndosi alisema kuwa , serikali tayari iko mbioni kuifungua zahanati hiyo ya Mlangali na taratibu zote zimekamilika  kilichobaki ni kupeleka mganga na madawa. Alisema kuwa mganga tayari huyo, lakini wanasubiri taratibu zingine zikamilike ili kuweza  zahanati hiyo kuanza kufanyakazi.
Alisema kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imetoa kibali cha kufunguliwa rasmi kwa  Zahanati ya Mlangali, ambayo ilikamilika tangu mwaka 2010.
“Wananchi wa  Kijiji cha Mlangali wasiwe na wasiwasi kabisa kwa sababu mganga wa zahanati hiyo  tayari na pesa tayari zipo kwa  ajili ya madawa kutoka Bohari ya Madawa ya Serikali (MSD),” alisema Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Ndosi.
Wakati huohuo, Zahanati ya Kijiji cha Mawengi nayo pia inakabiliwa na uhaba wa nyumba ya mganga  pamoja na choo cha uhakika, na kwa sasa zahanati hiyo inatumia choo cha muda.
Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...