Skip to main content

PEAWA SACCOS YAPATA HASARA YA SHILINGI MILIONI MOJA

Na Friday Simbaya, Songea


Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Peramiho (PEAWA SACCOS) kimepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni moja kwa mwaka unaoishia 31/12/2011 kutokana na sababu mbalimbali pamoja na baadhi ya wanachama kutorejesha mikopo kwa wakati.

Hayo yalibanishwa na meneja wa PEAWA SACCOS Nestory Mbena Jumamosi wakati akisoma taarifa ya ukaguzi kama ulivyokaguliwa na COASCO Songea kwenye Mkutano Mkuu wa Sita wa mwaka ulifanyika Peramiho katika Wilaya Songea, mkoani Ruvuma.

Alisema kuwa hasara hiyo pamoja na mambo mengine imetokana na wanachama waliokopa mikopo kuchelewesha kurejesha kwa wakati na wengine kutorejesha kabisa.

Meneja huyo aliongeza kuwa jumla yawadaiwa sugu 14 walipelekwa kwenye kampuni ya kukusanya madeni ya Yono ya Songea na baadhi ya wadaiwa wameanza kulipa baada ya kupelekwa mahakamani.

Alisema kuwa jumla ya mikopo iliyotolewa kwa wanachama katika kipindi cha kuishia Novemba 2012 ni 34 yenye thamani ya Tsh. 41,362,340/-.

“Jumla ya walioomba mikopo ni wanachama 57, lakini waliopata ni wanachama 34 na wasiopata mikopo ni wanachama 23 yenye thamani ya Tsh. 2,150,000/-,” alisema meneja hiyo wa PEAWA SACCOS.

Aidha, alisema kuwa chama hicho kimeweza kukuza hisa za wanachama kufikia Tsh. 17,680,000/-, akiba za wanachama kufikia Tsh. 29,252,955, na amana za wanachama kufikia Tsh. 4,688,750/ kunako Novemba 2012.

Naye mwenyekiti wa bodi wa chama hicho John Komba aliwasihi wanachama wote waliokopa mikopo warejeshe kwa wakati ili na wengine waweze kupata nafasi ya kukopa, ukizingatia maombi ya mikopo ni mengi na mtaji wa ndani unazidi kupungua.

Mpaka sasa mfuko wa ndani una shilingi milioni 31,362,340/- na mfuko wa nje ni shilingi milioni kumi, aliongeza mwenyekiti huyo wa bodi.

Alisema ili waweze kukuza mtaji wa ndani wanachama hawanabudi ya kuongeza hisa, akiba na amana hatimaye kuongeza nguvu mfuko wa ndani.

Chama cha PEWA SACCOS kumekusudia kukusanya jumla Tsh. 162, 800,000/-, katika kipindi cha Januari – Disemba 2013. Kazi zilizolengwa kutekelezwa kwa kipindi husika ni sambamba na kazi za kawaida za ofisi.

Makusanyo ya ndani yatakuwa ni Tsh. 82,030,000/- ambapo ni viingilio, hisa, akiba na amana na utawala wa majanga na vyanzo vya nje Tsh. 80,000,000/- kutoka SELF Tsh. 30,000,000/- na NSSF Tsh. 50,000,000/-.

PEAWA SACCOS ina jumla ya wanachama 120, ambapo wanaume ni 79 na wanawake ni 39 na vikundi vitano tangu kuanzishwa kwa SACCOS mnamo 2007 ikiwa na wanachama 40 waanzilishi.

Wakati huohuo, Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama (CCM), ambaye aliandaliwa kuwa mgeni rasmi kwa shughuli hiyo ameahidi kutoa msaada wa pikipiki na kuongeza mtaji wa ndani wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Peramiho (PEAWA SACCOS).

Mbunge huyo alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Sita wa mwaka wa chama hicho, ambapo hata hivyo aliwakilishwa na Diwani wa Kata ya Peramiho Izaki Alex Mwimba (CCM).

Awali, chama hicho kilimuomba mbunge huyo kuwatatulia baadhi ya changamoto ambazo chama hicho kinakabiliwa nazo ni kpungua kwa mtaji wa ndani na ukosefu wa usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kufuatilia miradi ya wakopaji pamoja na kukagua miradi hiyo mara kwa mara.

Alisema amepokea maombi ya chama hicho na kuongeza kuwa ataangalia uwezekano angalau kusaidia kimoja katika ya mambo mawili kati ya pikipiki na kuongeza mtaji wa ndani.

Hata hivyo, Diwani kwa Kata ya Peramiho alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa maeneo mbalimbali kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa (Saccos) ili waweze kukabiliana na tatizo la umasikini wa kipato, na kuongeza kuwa Saccos ni kuboko ya umasikini.











Mgeni Rasmi Diwani wa Kata ya Peramiho wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma Izaki Alex Mwimba, ambaye alimuakilisha Mbunge wa Jimbo la Peramiho (CCM) Jenista Mhagama akijiandaa kumpa mkono msoma risala Augusta Mwingira (Karani) baada ya kukabidhiwa risala wakati Mkutano Mkuu wa Sita wa mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (PEAWA SACCOS) uliyofaniyka Jumamosi tarehe 22/12/2012. Wanaoshuhidia ni mwenyekiti wa bodi John Komba, Mjumbe wa bodi Theresia Kapinga na meneja wa SACCOS Nestory Mbena. (Picha na Friday Simbaya)


Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Sita wa mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Peramiho (PEAWA SACCOS) wakifuatilia kwa umakini wakati meneja chama hicho Nestory Mbena (hayupo pichani) akisoma taarifa mbalimbali Jumamosi. (Picha na Friday Simbaya)

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Usimamizi katika Mkutano Mkuu wa Sita wa mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Peramiho

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...