Skip to main content

TUPSE: WAAJIRI NCHINI WANATAKIWA KULIPA MAPUNJO YA MISHAHARA KWA WAFANAYAKAZI

Na Friday Simbaya, Songea

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE) Taifa , Edson  Eliya Kivelege amewataka waajiri  nchini kuwalipa wafanyakazi mapunjo  ya mishahara  yanayotokana  kupandishwa kwa kima cha chini cha mishahara na serikali mwaka jana kabla  ya sheria haijakuchua mkondo wake.

Alisema mapunjo hayo yanatokana  na waajiri wengi wa makampuni ya walinzi  binafasi kutolipa viwango vipya vya mishahara baada ya serikali  kupitia bodi ya mishahara kutangaza kima cha chini kwa sekta zote mwezi wa saba mwaka 2013.

Katibu huyo wa TUPSE alisema hayo wakati wa  mahojiano maalum  na NIPASHE  alipofanya ziara yake katika Nyanda za Juu Kusini kwa lengo kukagua uhai wa chama  pamoja na kufanya maandalizi  ya  kufanyika kwa mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika hivi karibuni  jijini Dar es Salaam.
Aidha, Kivelege  alimteua  Zacharia Godwin Mfilinge kuwa mwakilishi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, ambayo ni  mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
Alisema  kuwa kuna baadhi ya makampuni ya walinzi binafsi ambao bado hawajaanza kutekeleza agizo la Serikali la  kupandisha mishahara ya wanafanyakazi kwa mfano, asilimia 46.4 kwa sekta binafsi kama ilivyopendekezwa na bodi ya mishahara nchini.

“Tutaanza kuwahesabia waajiri mapunjo kwa wafanyakazi kwa wanachama wote wa TUPSE kuanzia Januari mwaka huu. Serikali  kupitia bodi ya mishahara nchini litangaza viwango mbalimabli vya mishahara ikiwemo sekta binafsi, ambapo walitakiwa kuanza kulipa viwango hivyo mwisoni mwa mwezi wa saba mwaka jana, ” alifafanua Kivelege.

Aliongeza kuwa, “Makampuni madogo ya ulinzi ambayo yana wafanyakazi chini ya 100 watakiwa kulipa wafanyakazi kima cha chini cha mshahara cha shilingi 105,000/- na makampuni makubwa ambayo yana wafanyakazi zaidi ya 100, basi walipwe Shilingi Laki Moja na Nusu (150,000/-) kima cha chini cha mshahara yao!”

Wakati wa ziara yake katibu huyo wa TUPSE alitembelea pia Ofisi ya  Afisa wa Kazi mkoani wa Ruvuma pamoja na baadhi ya ,vyama vya wafanyakazi  vya TUICO, TIPWU, TULGU na TUGHE  vilivyopo mkoani hapa kwa lengo ya ushirikiano.

Katika hatua nyingine, Kivelege aliwataka waajiri kuwalipa wafanyakazi mishahara  ya kila mwezi kwa wakati ili kupunguza vitendo vya baadhi ya walinzi kushirki katika wizi malindoni.

“Unapowacheleweshia mishahara wafanyakazi (walinzi) unawatia katika vishawishi vya kuwa na tamaa ya kuwaibia matajiri kutokana  kuwa na maisha magumu. Waajiri wanatakiwa kuwalipa wafanyakazi mishahara kila mwezi na kwa wakati na kama watachelewa basi wawalipe kuanzia tarehe 5 ya mwezi unaofuata,” alisema.

Alisema pia kuwa waajiri  wanatakiwa kuwalipa wafanyakazi muda wa ziada (overtime) kama sheria inavyoelekeza .

“Sheria zipo zinazosimamia saa za kazi kwa sekta binafsi TanzaniaKipengele kidogo B cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 kinaelezea kuhusu saa za kazi. Kiwango cha juu kabisa cha saa za kazi ambacho mfanyakazi anaruhusiwa na sheria kufanya kazi ni saa 45 kwa juma ambayo ni sawa na saa tisa (9) kwa siku. Muda wa ziada zaidi ya saa 45 kwa juma lazima ulipwe kama saa za ziada,” alisisitiza katibu huyo.


Wakati huohuo, Katibu wa TUPSE taifa, Edson Kivelege alisema kuwa wakati wa ziara yake amebaini kuwepo akaunti nane (8) za benki za matawi ya chama hicho amabazo zilifunguliwa kinyuma na utaratibu wa TUPSE.  Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...