Skip to main content

mwanamke aiba mtoto


JESHI la polisi mkoani Rukwa linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye Magreth Juma (34)mkazi wa mtaa wa chanji katika manispaa ya sumbawanga kwa tuhuma za wizi wa mtoto mchanga mwenye umri wa siku mbili.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa asubuhi ya October 22 juzi nyumbani kwake maeneo ya chanji akiwa na mtoto huyo mwenye jinsia ya kike aikiwa ni muda mfupi tangu mtoto aibiwe toka kwa mama mzazi huko bangwe umbali wa takribani kilomita 15.

Inadaiwa kuwa awali taarifa zilifikishwa kituo cha polisi sumbawanga majira ya alfajili na mama wa mtoto huyo  Magreth Benisia (28)kuwa mtoto wake mchanga amepotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa nyumbani kwake ndipo polisi walianza msako mkali kwa kushirikiana na raia wema na muda mfupi baadaye waliweza kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mtoto nyumbani kwake.

Baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa katika maelezo yake ilibainika kuwa mama wa mtoto aliyeibiwa na ndugu wa mtuhumiwa waliwahi kuishi nyumba moja ya kupanga hivyo kupelekea mtuhumiwa kumfahamu vizuri mama huyo wa mtoto na hivyo kuwa rahisi kwake kutenda kosa hilo.

Uchunguzi ulibainisha kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mama wa watoto watatu aliozaa na mume wake mwingine mbali na Yule anayeishi naye sas,ameweza kuishi na mume wake wa sasa kwa zaidi ya miaka miwili bila kupata mtoto mwingine hali iliyoanza kuhatarisha ndoa yake kwani mwanaume huyo amekuwa akitaka kupata mtoto na ndo maana mama huyo aliamua kuiba mtoto katika harakati za kuilinda ndoa yake.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...