Skip to main content

PINDA : TUTAUNGANISHA NGUVU KWA MGOMBEA URAIS ATAKAYE TEULIWA NA CHAMA!


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsikiliza mwanafunzi wa shule ya sekondari Kiwere akifanya vitu vyake kwa kushirikiana wanafunzi wenzake katika maabara ya kemstri  alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa shuleni. Pinda leo alikagua ujenzi wa maabara na kufungua nyumba nne za walimu wa shule

hiyo zenye uwezo wa kubeba familia nane, halmashauri ya wilaya ya iringa katika jimbo la kalenga. 


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua mradi wa umwagiliaji pamoja na mashamba ya wakulima wa mpunga wa kijiji cha magozi, halmashauri ya wilaya iringa jimbo la isimani, akifuatana na  mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza akifuatia na kaimu mkuu wa wilaya ya iringa Gerald Guninita ambaye pia ni DC wa kilolo.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka watanzania hasa wana chama wa chama cha mapinduzi ( CCM)kuwa na subira katika kumpata mwanachama atakayefaa kusimama kugombea urais kupitia CCM mwaka huu.


“Kuwa tayari wengi sana wamejitangaza wazi wazi na wengine wamejitangaza kimya kimya kutaka kugombea Urais na kuwa yote heri ila chama kina utaratibu wake. Itafika wakati ambao kila chama kitasema huyu ndie mtu wetu ambaye atapambanana vyama vingine ...tunachosema sisi huyo atakayependekezwa ndie atakuwa mgombea wetu,"alisema Waziri Pinda Waziri
Pinda alitoa kauli hiyo jana wakati akiwahutubia wakazi wa tarafa ya Pawaga baada ya kuzindua skimu ya umwagiliji itakayowanufaisha wakazi wa vijiji vitatu kikiwemo cha Magozi,Ilolompya na Mkombilenga uliogharimu zaidi ya Tsh bilioni 1.6 fedha kutoka kwa wahisani na serikali.
Alisema kuwa utaratibu wa ndani ya chama ambacho wao ni watawala na wanaoendelea kuyafanya maendeleo yanaonekana watalazimika kumuunga mkono atakayeteuliwa na wale wote ambao hawajateuliwa watamuunga mkono atakayeteuliwa kwa makundi yote kuvunjwa na kuwa na Kundi moja pekee.
 Baada ya mgombea wa chama tawala kupatikana jukumu kubwa ni kuwaomba wapenzi wao wote kumchagua huyo aliyeteuliwa na chama.

Hivyo Waziri Pinda aliwataka wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura.
Alisema kuwa zoezi hilo ambalo litawahusu wale wote wenye miaka kuanzia 18 na kuendelea linataraji kuanza mwezi huu katika Mkoa wa Njombe na kuwa kila kata zoezi hilo litadumu kwa muda wa wiki mbili ama tatu .

" Nawaombeni kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na pia kuipigia kura katiba inayopendekezwa muda ukifika sisi tunaamini ni katiba bora ambayo imegusa makundi yote yakiwemo ya wafugaji na wakulima pamoja na makundi mengine," alisema Pinda.
Kuwa wapo wapotoshaji ambao watafika na kuwadanganya juu ya katiba hiyo inayopendekezwa na wasiwasikilize na kuongeza kuwa kazi kubwa imefanyika katika kuandaa katiba hiyo inayopendekezwa mbali ya wao (UKAWA) kutoka nje wakati wa bunge hilo la katiba lakini wajumbe waliobaki walifanya kazi nzuri ya kuandaa katiba hiyo inayopendekezwa hivyo kuwaomba wananchi kuipigia kura.

Katika hatua nyingine Waziri mkuu Pinda amewataka wakulima wa mpunga Pawaga katika kuepuka na migogoro kati yao na wafugaji kuweka utaratibu wa kukusanya majani ya mpunga na kuyapeleka majumbani kwao ili wafugaji wapate kununua kuliko kuyaacha mashambani na kuwafanya wafugaji kuingiza mifugo yao mashambani.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda yupo katika ziara ya siku tano mkoani Iringa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na baada ya hapo ataelekea mkoani Mbeya kuendelea na ziara.




Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...