Skip to main content

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAFUNGUA RASMI MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU


Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza na madereva bodaboda wa Kipunguni 'B' kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akizungumza na wananchi mbalimbali waliofanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda wakiume maeneo ya Kipunguni 'B' katika manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akitoa maelezo ya kina kuhusu faida na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF), akiongea na madereva wa bodaboda wa Kipungunu 'B' wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva hao.

Delphin Richard Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akisalimiana na muamuzi wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Madereva wa Bodaboda wa Kipunguni 'B' ambapo mfuko wa PSPF imedhamini mashindano hayo. Katikati ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa.



Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akitambulishwa wachezaji

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy akisalimiana na wachezaji katika ufunguzi wa ligi ya madereva bodaboda.

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza mmoja wa wazee kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF)

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akimjazia fomu ya Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa Kipunguni B wilaya ya Ilala jijini Dar mara baaada ya kupata elimu na kuridhia na huduma za mfuko huo.





Madereva bodaboda wawana mwitikio mkubwa wa kujiunga na mfuko wa PSPF kupitia (PSS) kwakujaza fomu za Uchangiaji wa Hiari

Afisa wa mfuko wa pensheni, Delphin Richard(kushoto) akimuonesha sehemu ya kuweka alama ya dole gumba mmoja wa madereva wakati wa ujazaji fomu za Uchangiaji wa Hiari


Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy(kulia) akiwajazia fomu za Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa Kipunguni B wakati wa mashindano ya mpira wa miguu katika eneo la Kipunguni B 





Madereva bodaboda wa mtaa wa Kipunguni 'B' kata ya Kivule manispaa ya Ilala wameanzisha ligi ya mpira wa miguu kwaajiri ya kuendeleza kujenga afya zao kwa michezo kwani michezo ni afya kwa wote, wakati wa ufunguzi huo wa ligi hiyo ya madereva bodaboda wadhamini wa ligi hiyo ambao ni Mfuko wa pensheni wa (PSPF)nao hawakuwa mbali kwaajiri ya kuwawezesha madereva hao kwa kipindi chote cha ligi hiyo.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi hiyo mgeni rasmi ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam Josephat Sylvery Tirumanywa amewaasa madereva hao kuwa waweze kucheza kwa amani michezo yote na pia waweze kuwa ni miongoni mwa watu watakao jiunga na na mfuko wa (PSPF) ka kupitia (PSS) kwaajiri ya kuendelea kupata huduma zilizo bora na zenye uhakika .


Pia Afisa masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Ismail Juma amesema wameamua kuungana na madeeva boda boda hao ili kuweza kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na kufaidika na mafao mbalimbali yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga na mfuko huo wataona matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao wanategemewa na familia zao hivyo kama Pspf wana mafao ambayo wataweza kujikwamua kama mafao ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la uzazi hata fau la nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala hauto jutia 


Naye Bw. Delphin Richard ambaye pia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) amewasisitiza madereva kutii sheria za barabarani na pia kuweza kucheza ligi hiyo kwa amani maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na upendo.


Hivyo kati ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya kazi kwa umoja na hivyo kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi yetu inajengwa na sisi watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi tuwapo barabarani,aliongeza kwa kuwapa shukrani madereva ya kuweza kuchagua mfuko wa pensheni wa Pspf kuwa wadhamini wa michuano hiyo kwani PSPF ipo kwaajiri ya kila mmoja na kuweza kuwaasa waweze kuwahamasisha watu mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha mabadiliko ya wananchi mbalimbali yanatokea kimaisha ,elimu,afya na mengine mengi.






Mfuko wa pensheni wa PSPF unafuraha ya kuwa kwa sasa wananchi wanajua kile kilicho sahihi nakuongeza kuwa wananchi mbalimbali waweze kufika maeneo ya kipunguni B ilikuweza kushirikiana na madereva hao kwa kuwashangilia wakati ligi ikiwa inaendelea na ligi hiyo itakayo dumu kwa takibani wiki moja.








Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...