Skip to main content

Msichana aongoza Form II kitaifa


Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde.

Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), limetangaza matokeo ya kidato cha pili huku msichana, Lineth Christopher kutoka Shule ya Sekondari ya St. Aloysius Girl’s ya mkoani Pwani, aking’ara kitaifa.

Matokeo hayo yalitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde, ambaye alisema waliofanya mtihani huo mwaka jana walikuwa ni wanafunzi 363,666 sawa na asilimia 91.66.

Alisema kati ya walioufanya mtihani huo, waliofaulu ni wanafunzi 324,068 sawa na asilimia 89.12, ambapo wasichana ni 164,547 sawa na asilimia 89.00 na wavulana ni 159.521 sawa na asilimia 89.24.

Dk. Msonde alisema wanafunzi 39,567 sawa na asilimia 10.88 walishindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya Kidato cha tatu; hivyo watarudia darasa wakati wanafunzi 33,104 sawa na asilimia 8.34 hawakufanya mtihani huo kwa sababu za utoro na magonjwa.

Alisema idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 155,667 sawa na asilimia 42.80 ambao kati yao wasichana ni 68,780 sawa na asilimia 37.20 na wavulana ni 86.887 sawa na asilimia 48.60.

Alisema katika ufaulu wa masomo, somo la hesabu limeshika mkia kwa kupata ufaulu wa asilimia 15.21 wa jumla wakati somo la Kiswahili limefanya vizuri kwa kuwa na ufaulu wa jasilimia 86.34.

Aliongeza kuwa ufaulu wa masomo ya siasa, historia, geografia, kingereza, fizikia, baiolojia, hesabu na utunzaji wa hesabu ‘Book Keeping’ umeshuka ukilinganishwa na mwaka 2014, hivyo aliomba juhudi za makusudi zifanyike.

Alisema ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya msingi ya Kiswahili, Biashara, na Kemia umepanda ikilinganishwa mitihani iliyopita.

Aidha, alisema wanaamini kuwa masomo yanayotegemea maabara yatafanya vizuri hapo baadaye kutokana na juhudi za serikali zinazofanyika za kuboresha maabara hizo.

WATAHINIWA KUMI BORA KITAIFA
Aliwataja kuwa ni Lineth aliyeng’ara kitaifa akifuatiwa na Jerry Panga (Marian Boys Pwani), Rhobi James Simba (Marian Girls) zote za Pwani.

Wengine ni Colin Emmanuel (Feza Boys Dares Salaam), Nickson Maro (Magnifcat Kilimanjaro), Diana Mwakibinga (Morning Star Mwanza), Elisha Peter (Buswelu Mwanza), Gaudencia Lwitakubi (Alliance Girls Mwanza), Fuad Thabit (Feza Boys Dar es Salaam) na Geraldina Kyanyaka (Canossa Dar es Salaam).

WASICHANA 10 BORA KITAIFA
Aliwataja wasichana bora kuwa ni Lineth, Rhobi, Diana, Gaudencia, Geraldina na Renata Chikola ambao wanatoka (St. Aloysius Girls).

Wengine ni Happyness Mwailunga (Canossa), Monica Tesha (St. Aloysius), Judith Amos (Precious Blood) na Amina Khalfan (Fedha Girls).

WAVULANA 10 BORA KITAIFA
Dk. Msonde aliwataja kuwa ni Jerry, Colin, Nickson, Elisha, Fuad, Mwinangwa Chibunde (Mwanza Alliance), Baraka Muhammed (Eagles Pwani), Joshua Kafula (Libermann Boys), Emmanuel Magombi (Morning Star), Frank Charles (Marist Boys).

SHULE 10 BORA
Katibu huyo alizitaja kuwa ni Mwanza Alliance, Mwanza Girls, Alliance Rock Army, St. Francis Girls, Bethel Sabs Girls, Don Bosco Seminary, Shamsiye Boys, Feza Boys, Feza girls na Canossa. 

SHULE 10 ZA MWISHO
Alizitaja kuwa ni Michenjele (Mtwara), Furaha (Dar es Salaam), Ndando (Tanga), Mlongwema (Tanga), Kwai (Tanga), Lionja (Lindi), Mkoreha (Mtwara), Mlungui (Tanga) Makong’onda (Mtwara) na Kwaluguru (Tanga).

Dk. Msonde alisema baraza linawasihi Maofisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wadhibiti ubora wa elimu kwa kufuatilia ili kuhakikisha ufundishji katika maeneo yaliyotakiwa kutiliwa mkazo unafanyika.

Pia aliwataka wazazi kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuhakikisha mazingira ya ufundishaji yanaboreshwa.
CHANZO: NIPASHE

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...