Skip to main content

OJADACT WALAANI SHERIA YA MAGAZETI YA MWAKA 1976




Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza.

Na:George Binagi-GB Pazzo +BINAGI MEDIA GROUP

Chama cha Waandishi wa Habari Wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Nchini OJADACT, Kimemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi yake ya kufanyia marekebisho sheria kandamizi kwa vyombo vya habari nchini, aliyoitoa wakati wa Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana.

Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko, ametoa ombi hilo hii leo mbele ya Wanahabari Jijini Mwanza, wakati akielezea hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali dhidi ya vyombo vya habari vinavyokiuka sheria katika utendaji wake wa kazi.

Soko alitolea mfano Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kupitia sura ya 229 kifungu cha 25 (1), kinachompa Mamlaka Waziri wa
Habari kulifungia gazeti lolote linalotoa habari zenye ukakasi, kuwa ni ishara ya ukandamizaji wa uhuru wa habari nchini, kwa kuwa kuwa sheria hiyo haitoi nafasi kwa chombo kinacholalamikiwa kujitetea ikizingatiwa kwamba Serikali ndiyo mlalamikaji na wakati huo huo mtoa hukumu. 

“Sheria ya Magazeti ni mbaya kwani haitoi nafasi kwa upande wa pili kujibu, huku serikali ikiwa ndiyo mlalamikaji na hapo hapo hakimu (Unfair game). Alitanabaisha Soko na kuongeza kuwa OJADACT inalaani matumizi ya sheria ya magazeti nchini ya mwaka 1976.

Wakati OJADACT ikitoa ombi hilo kwa Rais Dkt. Magufuli, baadhi ya Waandishi wa Habari Jijini Mwanza walikiri kuwepo kwa sheria zenye ukandamizaji wa Uhuru wa habari nchini ambapo wameomba sheria hizo kurekebishwa ili kukuza haki ya kutafuta na kutoa habari katika jamii.

Vyombo mbalimbali vya Habari nchini hususan Magazeti, vimekuwa vikikabiliwa na sheria kadhaa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa ya kwamba zinakiuka misingi ya uhuru wa habari ambapo ni hivi karibuni Serikali imelifungia gazeti la Mawio kuchapisha habari zake kutokana na kuchapisha taarifa zilizoelezwa kuwa na mkanganyiko katika jamii.



Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza.


Wanahabari


Kulia ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG






Kushoto ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG


Kushoto ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG


Baada ya Ojadact kutoa ombi lake kwa Mhe.Rais, Ikafuata Selfie


Kutoka Rock City Jijini Mwanza, Mimi ni GB Pazzo wa Binagi Media Group


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...