Skip to main content

MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YAFUTA KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI



Kulia ni Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG


Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, katika Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Christopher Ryoba Kangoye.

Katika kesi hiyo, wajibu maombi walikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe.John Heche (Chadema), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo mtoa maombi alikuwa akiiomba Mahakama kutengua matokeo ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo hilo kwa kuwa haukuwa huru na haki.

Baada ya Mahakama hiyo kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kusikiliza utetezi wa pande zote, iliamua kuifuta kesi hiyo ambayo ilikuwa ni nambari nne ya mwaka 2015 kutokana na hoja za mleta maombi kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kutoainisha majina ya waliokuwa wakilalamikiwa kuvuruga uchaguzi Jimboni humo.

Wakili wa mleta maombi Costantine Mutalemwa pamoja na Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja aliekuwa akisaidiana na Wakili Tundu Lisu katika kesi hiyo, wameelezea kuridhika na maamuzi ya Mahakama hiyo.

Nae Mwl. Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara, ameelezea kuwa na imani na Mahakama kutokana na maamuzi iliyoyatoa katika kesi hiyo pamoja na kesi nyingine zilizowahi kuamuliwa Mahakamani hapo na kuongeza kuwa sasa kazi imebaki moja kwa Mhe. Heche ambayo ni kuwatumikia wakazi wa Jimbo la Tarime Vijijini.

Kwa upande wake Mrimi Zabloni ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, ameelezea furaha kwa wananchi wa jimbo hilo huku akiwasihi kuweka imani na Mahakama hapa nchini katika kutoa maamuzi ya kesi mbalimbali.

Wananchi wengiMahakamani hapo kutoka Jimboni Tarime Vijijini walikuwa ni wafuasi wa Chadema
na wameonyesha kuyapokea maamuzi ya mahakama hiyo kwa furaha kubwa na kwamba wao waliamua ushindi wa Heche tangu Novemba 25 mwaka jana kwenye daftari la kupigia kura.












Kesi hiyo
ilisikilizwa January 19,2016 mwaka huu na kuahirishwa hadi juzi January 27,2015 kwa ajili
ya kutolewa maamuzi, lakini pia iliahirishwa hadi jana January 28,2016 ambapo maamuzi
yameweza kutolewa.


Mrimi Zabloni (Katikati) ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini akiongea na wanahabari


Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja akihojiwa na wanahabari


Wakili wa mleta maombi Costantine Mutalemwa akihojiwa na wanahabari


Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara na wafuasi wengine wa Chadema wakifurahia baada ya maamuzi ya Mahakama


Mahakamani kabla ya mashauri kutolewa


Mahakamani kabla ya mashauri kutolewa


Mahakamani kabla ya mashauri kutolewa


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...