Skip to main content

WANAWAKE MWANZA WATAKIWA KUTOBWETEKA ILI KUACHANA NA UTEGEMEZI KATIKA JAMII



Kulia ni Bi.Vileth Muhamusi ambae ni mmoja wa Wajasiriamali Jijini Mwanza akizungumza na Mwandishi wa taarifa hii, George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group (BMG).


Wanawake Mkoani Mwanza wametakiwa kutobweteka na kukaa majumbani bila kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali, kwa kuwa hatua hiyo inawafanya kuwa tegemezi katika jamii.

Bi.Vileth Muhamusi ambae ni mmoja wa wajasiriamali maarufu Jijini Mwanza, anaejishughulisha na biashara ya bustani hususan kuotesha miche mbalimbali ikiwemo miche ya mbao, matunda pamoja na kimvuli, aliyasema hayo jana wakati akizungumzia tatizo la ukosefu wa ajira kwa akina mama ambalo hivi sasa limegeuka janga kwa malezi ya watoto kutokana na baadhi yao kuwatumia watoto wao katika shughuli za kuomba omba mitaani ili kupata fedha za kujikimu kimaisha.

Bi.Muhamusi anaepatikana katika bustani zilizopo pembezoni mwa Ziwa Victoria katika barabara ya Makongoro Jijini Mwanza, alibainisha kwamba wanawake wanapaswa kuchukua hatua na kuachana na fikra za utegemezi, ikiwemo kujiunga na vikundi mbalimbali vya maendeleo, akitolea mfano kikundi chake kijulikanacho kama Mazingira Group, na kwamba kupitia vikundi hivyo wanawake wataweza kupiga hatua za kimaendeleo.

Alianza shughuli zake za kuotesha miche miaka mitano iliyopita, na ameweza kupata kipato cha kumuwezesha kujikimu kimaisha yeye pamoja na familia yake huku kubwa zaidi likiwa ni kumudu kuwasomesha watoto wake kutokana na biashara ya kuuza miche anayootesha, ambapo anabainisha kwamba biashara hiyo inalipa kwani kuna aina mbalimbali za miche ambayo ina soko kubwa, akitolea mfano miche ya Mitiki ambayo mche mmoja huuzwa hadi shilingi elfu tatu.

Hata hivyo bi.Muhanusi aliwatoa hofu wanawake juu ya suala la mitaji ambalo limekuwa likilalamikiwa na wengi, ambapo ametanabaisha kwamba shughuli nyingi za ujasiriamali ikiwemo ya bustani, hazigharimu mtaji mkubwa ikilinganisha na gharama za mahitaji yao ya kila siku kama vile gharama za saluni huku wakiwa hawana shughuli za kuwaingizia kipato.

Kauli ya Bi.Muhanusi iliungwa mkono na Edwin Soko ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Wajasiriamali Tanzania, aliebainisha kwamba ili wanawake waondokane na utegemezi ni vyema wakajitambua na kufungua fikra zao, kwani baadhi yao wamekuwa wakiwekeza katika matumizi mabaya ya fedha ikiwemo kutumia hadi shilingi elfu sabini kwa ajili ya urembo huku wakiwa
hawana shughuli za uzalishaji mali, jambo ambalo linawakwamisha wengi wao kupiga
hatua za kimaendeleo. 




Mmoja wa Vijana wanaootesha mbegu


Miche ya aina mbalimbali


Ukiona njiti za Viberiti, basi tambua kwamba zinatokana na miti hii ambayo inajulikana kwa jina la Mitiki. Miti ya Mitiki pia ni mizuri na imara kwa ajili ya mbao.

Picha na Hamza Makuza, BMG Mwanza.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...