Skip to main content

DC. BAGAMOYO AKABIDHI MADAWATI 50 KWA SHULE MBILI ZA MSINGI


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed Mwanga,kulia mwenye miwani. akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Majengo madawati.


Na Athumani Shomari, Bagamoyo.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid HEmedi Mwanga amekabidhi madawati 50 kwa shule mbili za msingi ikiwa ni mkakati wa mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everisti Ndikilo wa kuondoa uhaba wa madawati unaozikabili shule za mkoa wa Pwani.

Madawati hayo 50 yenye thamani ya shilingi milioni nne yamekabidhiwa kwa shule za msingi Majengo na Mbaruku zote za Bagamoyo mjini.

Majidi amewashukuru wadau wa maendeleo ya elimu wilayani Bagamoyo ikiwemo kampuni ya Kirai Pateli ambayo ndiyo imetoa madawati hayo 50 ili kuondoa tatizo hilo kwa shule za serikali huku Shubashi Pateli amtoa ahadi ya kutengeneza madawati yote yanayohitajika kwa shule za Bagamoyo ambayo ni 1,353. 

Ili kwenda sambamba na agizo la mkuu wa mkoa wa Pwani ambae amesema mpaka kufikia tarehe 30 may shule zote za mkoa wa Pwani ziondokane na uhaba wa madawati.

Aidha, amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo ya elimu wilayani Bagamoyo kuendelea kuchangia mahitaji mbalimbali ya elimu katika wilaya ya Bagamoyo na kuongeza kuwa mara baada ya kukamilisha madawati yanayhitajika kwa shule zote wilaya imepanga kuanza kazi ya umaliziaji wa maabara za shule hivyo michango inahitajika kutoka kwa wadau mbalimbali ili kufikia malengo.

Kati ya madawati hayo 50 ishirini na manane yamekabidhiwa kwa shule ya msingi Majengo huku Ishirini na mawili kukabidhiwa kwa shule ya msingi Mbaruku na kumaliza tatizo la madawati kwa shule hiyo ya Mbaruku.

Awali akiongea mbele ya mkuu wa wilaya mkuu wa shule ya msingi Majengo Andulile Lukama amesema shule ya Majengo ina madawati 250 na ina upungufu wa madawati 109 na kwamba inakabiliwa pia na upungufu wa vyumba vya kusomea hali inayopelekea wanafunzi kuingia kwa zamu ambapo darasa la nne na la sita wanalazimika kutoka saa saba ili kuwapisha darasa la tano na la tatu.

Aidha, mwalimu mkuu huyo wa shule ya msingi Majengo Andulile Lukama na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Anna Kisonso wamemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa juhudi ya kutafuta wahisani ili kusaidia kuondoa changamoto zinazozikabili shule za serikali wilayani hapa.

Wakati huohuo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed Mwanga, amewataka walimu wakuu wa shule zote za Bagamoyo kuacha tabia ya kutumia madawati ya shule kwa shughuli za mikutano ya hadahara.

Majid amesema kuwa madawati ni kwaajili ya wanafunzi kusomea hivyo ni marufuku kuytatumia kwaajili mikutano ambayo haihusiani na shule.

Amesema kitendo cha kutoa madawati nje kwaajili ya mikuatano mbalimbali kinachangia uharibifu wa madawati hayo na baadae kupelekea usumbufu kwa wanafunzi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...