Skip to main content

SHEIKH JALALA AWAKUTANISHA MASHEIKH, MAIMAMU WA MADHEHEBU TOFAUTI, WAJADILI DHULMA DHIDI YA WAPALESTINA


Kiongozi Mkuu wa Waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu siku ya Quds inayokumbukwa na Waislamu wote Duniani kote.Matembezi ya siku hiyo hapa nchini yanatarajiwa kuwa Tarehe mosi mwezi ujao.


Masheikh na Maimamu wakiwa katika semina maalum inayohusu kutafakari juu ya kadhia ya Palestina, semina hiyo ilifanyika katika Msikiti wa Al Qadir Kigogo Post Daresalaam.


Kiongozi Mkuu wa Waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema kila mwanadamu anawajibu kupiga vita dhidi ya matendo ya dhulma wanayofanyiwa Wapalestina.


Hayo ameyasema jana katika semina maalum ya Quds, iliyowakutanisha Viongozi wa Dini, mbalimbali wakiwamo Maimam, Masheikh na Maustadhi kutoka Madhehebu mbalimbali ya Kiislam, semina iliyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.


Katika semina hiyo ya siku moja iliyokuwa na dhamira ya kujadili umuhimu wa kadhia ya Palestina na jinsi inavyotuunganisha waislamu kama kadhia mama, Jalala ametumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa umma kuwa kuna haja ya Waislamu kupinga matendo wanayofanyiwa wapalestina kwani suala hilo halina mahusiano na uarabu na Siasa.


Amesema wapalestina wanafanyiwa uvamizi katika nchi yao, wamekuwa hawana Amani kama Nchi zingine na kwamba jambo hilo halikubaliki ni lazima lipigiwe kelele ili Wapalestina waweze kupata haki zao za msingi.


“Sisi kama waislam tumeelekezwa juu ya kujali mambo ya Waislamu wenzetu, lakini nataka niseme wanaopata tabu pale Palestina si Waislamu peke yao, kuna Wakristo pia niwaombe Watanzania kwa ujumla kufahamu hilo na kuwaombea wenzetu wawe na Amani”Alisema Sheikh Jalala


Amesema pindi Sauti inapopazwa ndivyo vyombo vya umoja wa mataifa ukavyodhi kuelelewa ukubwa wa Tatizo na hivyo kuweza kutoa shuruhisho muhimu kwa mustakabali wa Amani ya Palestina


“Tunaomba vyombo vya umoja wa mataifa, Watanzania Waislamu na wasio Waislamu kuunga mkono jitihada za kupinga dhulma dhidi ya watu wa Palestina, kwa kuwaombea ili nao waweze kufaidi keki ya Amani kama Watanzania wanavyofanya.


Aidha amesema Wapalestina wakristo na waislam wakae vizuri na dini zingine kama kama ilivyo Tanzania, na hilo linawezekana kama dunia itaamua kupiga kelele juu ya umuhimu wa Wapalestina kupewa haki zao.

“Tungependa Palestina tuione ina Amani kama Tanzania, Nchi hii inajulikana kwamba ni kisiwa cha amani, ni mahala pa maelewano, katika historia yake ya Tanzania haitambui ubaguzi na hivyohivyo palestina iwe ni mahala pa amani, iwe ni mahala hapana ubaguzi, watu wote wakae pamoja, wakae kwa maelewano, dhulma isambaratike, dhulma iondoke” Alisema Jalala


Alisema unapoingalia historia ya palestina na yanayojiri katika ardhi ya palestina ni dhulma unyonyaji, ukandamizaji ambao ni makosa na wala hauruhusiwi kuunyamazia kimya si kwa Waislamu au Wasiokuwa Waislamu Waislamu na Wasio Waislamu wanaikukumbuka na kuadhimisha siku ya Quds Duniani ambayo kwa maana nyingine wanaadhimisha na kuikumbuka palestina (Msikiti mtukufu wa Quds na ardhi tukufu), Kuikumbuka palestina na siku ya Quds ni jambo ambalola kitabia(kiakhlaq), pili ni jambo la kidini na tatu ni jambo la kiuwanaadam. ‪





Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...