Skip to main content

KINA DADA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI UVCCM



Katibu wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Iringa (UVCCM) James Mgego (pichani) amewahimiza vijana wa jumuiya hiyo kujitokeza kugombea nafasi za uongozi hasa wa kina dada ambao wako nyuma kuchangamkia fursa hizo.

Akoingea na SIMBAYABLOG jana katibu huyo alisema kuwa tangu kuanza kwa zoezi hilo ngazi ya mkoa ni vijana 44 tu kati yao wakina dada ni wanne, ikizingatia kuwa mwaka 2017 wa uchaguzi ndani CCM.

Mgego alisema kuwa jumuiya hiyo ni jumuiya ya vijana ya CCM ni kwa ajili ya vijana wote wakiume na wakike lakini inashangaza kuona dada zetu wanakuwa nyuma kuchangamkia fursa za kugombea nafasi za uomgozi ndani ya umoja huo.

Pia katibu huyo aliwataka vijana kuendelea kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na kutowasikiliza watu ambao wapo kuona CCM inakwama katika uchaguzi huo wa ndani ya chama.

Alisema kuwa zoezi la utoaji fomu za uongozi wa UVCCM ngazi ya mkoa ilianza tarehe 02.07.2017 na kukamilika tarehe 10.07.2017 katika ofisi ya UVCCM mkoa wa Iringa na katika ngazi ya wilaya zoezi pia linaendelea na kuongoza kuwa fomu hizo zinatolewa bila malipo.

Mgego alizitaja nafasi hizo za uongozi zinagombewa kuwa ni mwenyekiti UVCCM Mkoa, Mjumbe wa mkutano Mkuu CCM Taifa, Mjumbe Baraza Kuu UVCCM, Mjumbe Mmoja Kuwakilisha UWT, Mjumbe Mmoja kuwakilisha Wazazi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Mkoa na Mjumbe wa mkutano wa UVCCM Taifa.

“Tulianza na uchaguzi wa mashina umekamilika, ukafuata wa ngazi ya kata naomemalizika na vikao vyake vinaendelea kuchuja wagombea na sasa ni uchaguzi wa UVCCM ngazi mkoa na taifa unaendelea…”alisema katibu huyo.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...