Skip to main content

SALIM ABRI (ASAS) AIZINDUA KAMPENI ZA CCM KILOLO, AMTANGAZA DR. RITTA KABATI


Kilolo, Iringa – Septemba 14, 2025

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC) na Mratibu wa Kampeni Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Salim Abri maarufu kama Asas, leo amezindua rasmi kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilolo pamoja na wagombea wa nafasi za udiwani kupitia CCM katika jimbo hilo.

Mgombea Ubunge wa Kilolo, Dr. Ritta Kabati, ndiye mwanamke pekee kati ya wagombea wa majimbo saba ya ubunge mkoani Iringa kupitia CCM. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dr. Kabati aliishukuru CCM kwa kuendelea kumuamini na kumpa jukumu la kupeperusha bendera ya chama, akisisitiza kuwa uzoefu wake wa miaka 15 kama Mbunge wa Viti Maalum umemwandaa vyema kuwatumikia wananchi wa Kilolo kwa bidii, uadilifu na upendo.

Ameahidi kutekeleza kikamilifu Ilani ya CCM 2025–2030 bila upendeleo, huku akihimiza mshikamano kati ya viongozi na wananchi, kuvunja makundi ya kijamii na kisiasa, na kuharakisha maendeleo ya jimbo hilo. Aliwaomba wananchi kumpigia kura yeye, Rais Samia Suluhu Hassan na madiwani wote wa CCM.

Kwa upande wake, Salim Abri (Asas) alisema Dr. Kabati si mgeni katika uongozi, akibainisha kuwa Kilolo imepata mgombea mwanamke mwenye maono, uzoefu na uwezo wa kushughulikia changamoto za wananchi. Alisisitiza kuwa Dr. Kabati amejikita katika kupigania huduma bora za afya, upatikanaji wa maji, kupambana na rushwa, na kusaidia makundi maalum kama watu wenye ulemavu.





Aidha, Abri alitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana Kilolo chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, yakiwemo ujenzi wa vituo vya afya vitano, zahanati kumi, vyumba vya madarasa 493, vyoo 352, miradi ya maji safi, pamoja na shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa. Alisema mafanikio hayo ni ushahidi wa utekelezaji bora wa ilani ya CCM unaoendelea kuleta matokeo chanya kwa wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo, John Kiteve, alisema wananchi wa Kilolo wako tayari kuiunga mkono CCM kwa kura zote, akibainisha kuwa ilani ya mwaka 2020–2025 imetekelezwa kwa mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali, huku ilani ya 2025–2030 ikilenga zaidi kutatua changamoto za wananchi na kuboresha maisha yao.




 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...