Skip to main content

ASAS AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU VURUGU ZA UCHAGUZI


MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, huku akiwatoa hofu juu ya uvumi unaoenezwa mitandaoni kuhusu uwepo wa vurugu siku ya uchaguzi huo.

Asas amesema kumekuwepo na taarifa zisizo sahihi kutoka kwa baadhi ya watu, ndani na nje ya nchi, wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasisha maandamano na kuchochea vurugu ambazo zinaweza kuhatarisha amani na kuathiri zoezi la uchaguzi.

Akihutubia maelfu ya wanachama na wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM Jimbo la Mafinga Mjini, uliofanyika katika kijiji cha Ugute, kata ya Isalavanu, Halmashauri ya Mji Mafinga, Asas aliwahakikishia wananchi kuwa nchi ipo salama na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu kulinda amani.

“Nataraji katika siku hizi mbili mtajitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 29. Msiogope wala kuwa na hofu, amani ipo na kutakuwa na ulinzi wa kutosha. Nchi yetu imetulia — hayo yote ni maneno ya mitaani,” alisema Asas.

Amesisitiza kuwa Tanzania ipo kwenye mikono salama ya vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo wananchi wanapaswa kutumia hali hiyo kama motisha wa kushiriki uchaguzi na kutimiza haki yao ya kikatiba.








Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Dickson Lutevele maarufu kama Villa, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kama ishara ya shukrani kwa Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo hilo.

Aidha, aliwasisitiza wananchi wote—bila kujali itikadi za kisiasa au imani za kidini—kudumisha amani ambayo ndiyo msingi wa maendeleo endelevu.

“Ni imani yangu kuwa Mufindi kwa mara nyingine tena tutaongoza kwa wingi wa kura kukichagua Chama Cha Mapinduzi kama kawaida yetu,” alisema Villa.


 

Asas urges voters to turn out in large numbers, dismisses election violence fears


 

Iringa. A member of the CCM Central Committee (MCC), Salim Abri Asas, has urged Tanzanians to turn out in large numbers to cast their votes in the upcoming General Election on October 29, assuring them that the country remains peaceful and well-secured.

Mr. Asas dismissed circulating rumours on social media suggesting that there might be violence on election day, saying such claims are being spread by individuals with ill intentions to create fear and discourage voter participation.

He said in recent weeks, there have been coordinated attempts by certain groups, both within and outside the country, to incite youths and other sections of the community to engage in demonstrations and acts that could disrupt peace and affect the election process.

Speaking during a well-attended CCM rally to close the party’s campaigns for Mafinga Urban Constituency, held at Ugute Village in Isalavanu Ward, Mr. Asas assured citizens that the security organs are fully prepared to maintain order and safety throughout the election period.

“I expect all of you to turn out in large numbers to vote on October 29. Do not be afraid or worried — peace prevails, and there will be enough security everywhere. Our country is calm; those stories are just rumours,” said Asas.

He added that Tanzania is in safe hands under its security institutions, urging citizens to take advantage of the prevailing peace to fulfil their constitutional right to vote.

On his part, Dickson Lutevele, popularly known as Villa, who is vying for the Mafinga Urban parliamentary seat, expressed confidence that residents will show up in large numbers to vote as a sign of appreciation for the government’s development efforts in the area.

He emphasized that regardless of political affiliation or religious belief, citizens should prioritize peace, which he described as the foundation of inclusive and sustainable development.

“I strongly believe that once again, Mufindi will lead with overwhelming votes in favour of the CCM, as has always been our tradition,” said Villa.


 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...