Skip to main content

INEC YAWATAKA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUACHA MAZOEA, WAZINGATIE SHERIA


Iringa. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele, amewataka wasimamizi wa uchaguzi nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria za uchaguzi na kanuni zake, akisisitiza kuwa hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea bali kwa kufuata maelekezo ya Tume.

Jaji Mwambegele ametoa wito huo Januari 24, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi ngazi ya jimbo na kata, maafisa uchaguzi, maafisa ununuzi pamoja na wahasibu. Mafunzo hayo yanafanyika kuanzia Januari 24 hadi 26, 2026.

Akizungumza katika hafla hiyo, amewapongeza wajumbe wa Tume pamoja na waratibu wa uchaguzi wa Mikoa ya Songwe na Ruvuma kwa uteuzi wao, akisema umezingatia weledi, haki, uwazi na matakwa ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Amesema matarajio ya Tume ni kuona chaguzi zinaendeshwa kwa uadilifu wa hali ya juu, huku akisisitiza umuhimu wa wasimamizi wa uchaguzi kuheshimu viapo walivyoapa na kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume.

“Msifanye kazi kwa mazoea. Kila uchaguzi una mazingira na changamoto zake tofauti,” amesisitiza Jaji Mwambegele.

Aidha, amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili pamoja na wadau wengine wa uchaguzi katika masuala muhimu ya kiuchaguzi. Pia amesisitiza umuhimu wa kuyafahamu vizuri maeneo yatakayohusika na uchaguzi, ikiwemo miundombinu ya kufikia vituo vya kupigia kura.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wasimamizi wa uchaguzi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, hususan katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Peramiho na Uchaguzi wa Diwani Kata ya Shiwinga, Mkoa wa Songwe.

Uchaguzi huo umeitishwa kufuatia vifo vya Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Muhagama, na Diwani wa Kata ya Shiwinga, Lusekelo Mwalukomo.





Kwa upande wake, Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Ruvuma, Athumani Kateula, amewahimiza wananchi wenye sifa katika Jimbo la Peramiho kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi ya ubunge, kushiriki kikamilifu katika kampeni na hatimaye kujitokeza siku ya uchaguzi kuchagua kiongozi mwenye sifa.

Naye Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbozi, Danny Tweve, amesema maandalizi ya Uchaguzi wa Diwani Kata ya Shiwinga yanaendelea vizuri, akibainisha kuwa wamejipanga kuhakikisha hatua zote za uchaguzi—kuanzia uteuzi wa wagombea, kampeni hadi siku ya kupiga kura—zinasimamiwa kwa kuzingatia Katiba na sheria za nchi.

Kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mafunzo hayo, wasimamizi wa uchaguzi walikula kiapo cha kujitoa katika uanachama wa vyama vya siasa, hatua iliyolenga kuimarisha misingi ya uwazi, haki na kutokuegemea upande wowote katika usimamizi wa chaguzi.














 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...