Skip to main content

Halmashauri Ya Manispaa Ya Iringa Yashauriwa Kudhibiti Mapato Ya Vibali Vya Ujenzi






Iringa. Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeshauriwa kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato yatokanayo na vibali vya ujenzi ili kuongeza mapato na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ushauri huo umetolewa leo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Sifaeli Kivamba, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Kivamba alisema halmashauri inapoteza mapato kutokana na kutosimamia ipasavyo utoaji na matumizi ya vibali vya ujenzi, huku ujenzi ukiendelea katika maeneo mbalimbali bila vibali halali.

“Kuna ujenzi unaendelea kila siku lakini wengi hawana vibali, hali ambayo inainyima Serikali mapato. Naomba waheshimiwa madiwani mfuatilie suala hili katika maeneo yenu kwa kuhoji kila anayeendelea na ujenzi kama ana kibali,” alisema Kivamba.



Hata hivyo, aliipongeza Baraza la Madiwani kwa kusimamia vyema muda wa mkutano huo uliodumu kwa saa moja na nusu pekee, ikilinganishwa na awali ambapo vikao vilikuwa vikichukua hadi saa sita. Alisema hali hiyo imetokana na mafunzo (semina) waliyopewa madiwani kuhusu uendeshaji wa vikao pamoja na matumizi ya vishikwambi (tablets).

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada, aliwataka wafanyabiashara ndogondogo wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi kuondoka mara moja na kuelekea katika maeneo waliopangiwa ili kuweka mji katika mpangilio mzuri na kulinda mazingira.

Ngwada alisema hayo leo wakati akijibu swali la Diwani wa Viti Maalum Kanda ya Mlandege, Husna Mtasiwa, katika kipindi cha maswali na majibu, akisisitiza kuwa wafanyabiashara hao hawaruhusiwi kufanya biashara barabarani au maeneo mengine yasiyo rasmi.


Awali, Mtasiwa alihoji ni lini halmashauri itawawezesha wafanyabiashara hao kuhamia katika maeneo rasmi baada ya kuondolewa katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Naye Diwani wa Kata ya Mlandege, Wakili Dickson Chaula, aliuliza ni lini halmashauri itaboresha mazingira ya ukusanyaji mapato katika Soko la Kisasa la Mlandege maarufu Soko la Mwamwindi.

Akijibu swali hilo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ambaye pia ni Katibu wa Baraza, Zaina Mlawa, alisema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ukusanyaji mapato kwa kuwataka wafanyabiashara wote waliopo sokoni hapo kuzingatia mikataba yao ili kuwezesha ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi kwa maendeleo ya manispaa.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...