Skip to main content

Aomba Kuteuliwa Ubunge, Amuomba Samia Suluhu Hassan Amkumbuke


Iringa. Mwenyekiti wa Wazazi Wenye Watoto Wenye Ulemavu Mkoa wa Iringa, Bw. Zawadi Msigalla, amesema ana ndoto ya siku moja kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwatetea watu wenye ulemavu na makundi maalum, akimuomba Rais Samia Suluhu Hassan amkumbuke katika nafasi 10 za uteuzi wa wabunge.

Bw. Msigalla, ambaye ni mtu mwenye ulemavu, amesema dhamira yake ya kuingia bungeni inatokana na uzoefu wake wa muda mrefu katika utetezi wa haki za watoto wenye ulemavu na wazazi wao, akibainisha kuwa sauti ya kundi hilo bado haijapewa uzito unaostahili katika vyombo vya maamuzi.

“Nina ndoto ya kuwa Mbunge ili niweze kuzungumza kwa niaba ya wazazi na watoto wenye ulemavu. Tuna changamoto nyingi zinazohitaji uwakilishi wa moja kwa moja,” amesema Msigalla.

Akizungumza na Pamlomo- Sauti Ya Jamii mesema anaamini kuwa kupitia nafasi za uteuzi wa Rais, bado kuna fursa kwa watu wenye ulemavu na watetezi wao kushiriki kikamilifu katika kutunga na kusimamia sheria.

Mbali na kuwa mwenyekiti wa wazazi hao, Msigalla pia ni Afisa Mhamasishaji wa shirika lisilo la kiserikali la Kiitaliano la Nyumba Ali, linalojihusisha na miradi ya kijamii ikiwemo elimu jumuishi, afya na ustawi wa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.

Kupitia nafasi hiyo, amesema amekuwa akihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwajumuisha watoto wenye ulemavu katika shule za kawaida, kupambana na unyanyapaa na kuhakikisha wanapata huduma stahiki za afya na kijamii.

Msigalla amesema iwapo atapata uteuzi, atapigania kuimarishwa kwa sera na sheria zinazolinda haki za watu wenye ulemavu, kuongeza bajeti kwa ajili ya elimu jumuishi pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za tiba na vifaa saidizi.

“Watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa. Tunachohitaji ni kuaminiwa na kupewa nafasi. Nikiingia bungeni, nitakuwa sauti ya wale ambao mara nyingi hawasikiki,” amesema.

Alizaliwa mwaka 1998 wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, kabla ya kuhamia Iringa alipokutana na shirika la Nyumba Ali lililomsaidia katika masomo yake. Amesema alikumbana na changamoto nyingi za kukataliwa na shule kutokana na ulemavu wake.

“Nimesoma kwa msaada wa shirika la Nyumba Ali. Bila wao nisingeweza kusoma kwa sababu baadhi ya shule zilinikataa kutokana na hali yangu,” amesema.

Msigalla alihitimu mwaka 2022 katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha (RUCU) aliposomea sheria ngazi ya cheti, na baadaye kuajiriwa na shirika hilo kama Afisa Mhamasishaji.

Akizungumzia maisha yake binafsi, amesema ndoa yake na mkewe, Atupenda Valentino Ng’ande, imekuwa ushuhuda kwamba watu wenye ulemavu wanaweza kuishi maisha ya kawaida na yenye heshima kama wengine.

Kwa upande wake, Bi. Ng’ande amesema licha ya changamoto za maneno kutoka kwa baadhi ya watu, ameamua kusimama imara na kuonesha kuwa ndoa yao imejengwa katika upendo na heshima.

Baadhi ya wazazi wa watoto wenye ulemavu mkoani Iringa wameeleza kumuunga mkono Msigalla, wakisema uzoefu wake wa moja kwa moja katika kukabiliana na changamoto za malezi na utetezi unamfanya kuwa kiongozi anayeelewa mahitaji halisi ya kundi hilo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais ana mamlaka ya kuteua wabunge 10 kwa lengo la kuongeza uwakilishi wa makundi mbalimbali bungeni.

Msigalla anaamini kuwa uteuzi wa mtu mwenye ulemavu au mtetezi wao utakuwa ishara ya kuimarisha usawa na ujumuishaji katika uongozi wa kitaifa.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...