Skip to main content

RUCU Yazindua Tovuti Mpya Yenye Teknolojia Ya Akili Unde



Iringa. Chuo Kikuu cha Ruaha Catholic University (RUCU) mkoani Iringa kimezindua rasmi tovuti mpya ya kisasa iliyounganishwa na teknolojia ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI) kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa na huduma kwa wanafunzi, wazazi na wadau wa elimu.

Akizindua tovuti hiyo Machi 11, 2026, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Chrispina Lekule, alisema RUCU kama taasisi ya elimu ya juu inaendelea kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani.

Alisema kupitia maboresho na tafiti mbalimbali, chuo hicho kimefanikiwa kubuni tovuti ya kisasa yenye muundo unaorahisisha matumizi kwa watumiaji kupitia simu za mkononi au kompyuta.

“Tovuti hii mpya (www.rucu.ac.tz) imeboreshwa kwa muundo wa kisasa unaorahisisha matumizi kwa watumiaji kupitia simu au kompyuta. Pia imeunganishwa na teknolojia inayomwezesha mtumiaji kuuliza maswali mbalimbali kuhusu RUCU na kupata majibu sahihi papo hapo,” alisema Profesa Lekule.

Alifafanua kuwa teknolojia hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa mawasiliano kati ya chuo na wadau wake pamoja na kuboresha utoaji wa huduma kwa wanafunzi, wazazi na walezi.

Kupitia tovuti hiyo, watumiaji wataweza kupata taarifa mbalimbali ikiwemo programu za masomo na ada zake, uongozi wa chuo, huduma za wanafunzi pamoja na fursa za ushirikiano na uwezekano wa kupanga miadi na viongozi wa chuo.

Aidha, tovuti hiyo pia itaunganisha wahitimu wa chuo (alumni), kuonesha miradi mbalimbali inayotekelezwa na RUCU, machapisho ya kitaaluma, shughuli za huduma kwa jamii pamoja na maisha ya wanafunzi chuoni ikiwemo vipaji na bunifu zao.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Tovuti hiyo, Dk Willy Migodela, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shahada za Awali, tovuti hiyo inalenga kuifanya RUCU kuwa karibu zaidi na jamii kwa kutumia teknolojia ya kisasa, sambamba na kutoa jukwaa la kuonesha mchango wa chuo katika maendeleo ya elimu, tafiti, ubunifu na huduma kwa jamii.

Alisema tovuti hiyo itarahisisha upatikanaji wa taarifa kwa haraka bila kulazimika kusafiri au kupiga simu.

“Katika dunia ya sasa, kuokoa muda na gharama ni jambo muhimu. Badala ya mtu kusafiri kutoka mbali kuja Iringa kuuliza maswali, anaweza kuuliza moja kwa moja kupitia tovuti na kupata majibu papo hapo,” alisema Dk Migodela.

Aliongeza kuwa hata badala ya kupiga simu, mtu anaweza kuuliza maswali mbalimbali kupitia tovuti hiyo na hivyo kuokoa gharama za mawasiliano.

Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa RUCU (RUCUSO), Mussa Nelson Labia, alisema tovuti hiyo itasaidia kuitangaza RUCU ndani na nje ya nchi pamoja na kuwawezesha wanafunzi kupata huduma mbalimbali kwa urahisi.


 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...