Skip to main content

Ushiriki wa Baba katika Malezi ni Nguzo ya Kufikia Dira ya Taifa 2050 – RC Kheri James


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema ushiriki wa baba katika malezi na makuzi ya watoto ni muhimu katika kujenga kizazi chenye maadili mema na uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa, hatua inayosaidia kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.

RC James alitoa kauli hiyo wakati akifungua mdahalo wa pamoja wa kujadili ajenda ya malezi uliofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (MUCE) mkoani Iringa, aliyoandaliwa na taasisi ya Montessori Community of Tanzania (MCT) kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kupitia Idara ya Ustawi wa jamii mkoa.

Alisema baba ana nafasi kubwa katika malezi ya watoto na kwamba ushiriki wake husaidia watoto kukua katika mazingira ya upendo, ulinzi na maadili mema, hali inayochangia kujenga jamii imara na yenye uwajibikaji.

“Malezi bora ya mtoto hayawezi kufanywa na mzazi mmoja pekee. Ushirikiano wa baba na mama ni muhimu ili mtoto akue katika mazingira yanayomjengea nidhamu, maadili na uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa,” alisema RC James.

Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Iringa Martin Chuwa alibainisha kuwa katika baadhi ya familia, baba wamekuwa wakiachwa nyuma au kujiondoa katika majukumu ya malezi, jambo ambalo linaathiri ukuaji na maendeleo ya watoto.

Alisisitiza umuhimu wa jamii kuhamasisha ushiriki wa baba katika malezi ili kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yatakayowaandaa kuwa raia wema na wenye mchango katika maendeleo ya nchi.

Mdahalo huo uliwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wasomi, wanafunzi na viongozi wa jamii kwa lengo la kujadili namna bora ya kuimarisha malezi ya watoto na kuwajenga katika misingi imara ya maadili na uwajibikaji.

 












 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...