Skip to main content

Askari Polisi Ahukumiwa Miaka Miwili Jela kwa Kuua Bila Kukusudia Iringa


Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa, imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela askari polisi, Sajenti Rogers Mmari, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kuua bila kukusudia katika tukio lililosababisha kifo cha Nashon Kiyeyeu (23).

Hukumu hiyo ilitolewa Machi 19, 2026 na Jaji Angaza Mwipopo, kufuatia mahakama kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka uliothibitisha kuwa mshtakiwa alihusika na kifo cha Kiyeyeu, mkazi wa Nyamhanga, Manispaa ya Iringa.

Katika kesi hiyo, ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 14, 2024 katika eneo la Ipogoro, ambapo marehemu alishambuliwa na askari huyo kwa kushirikiana na mgambo, Thomas Mkembela, hali iliyosababisha kupoteza maisha yake. Tukio hilo lilihusishwa na tuhuma za wizi wa simu ya mkononi inayodaiwa kuwa ya Beatrice Baraka Kimata.

Akisoma hukumu, Jaji Mwipopo alisema ushahidi uliowasilishwa haukuonesha kuwepo kwa nia ya moja kwa moja ya kuua, hivyo mahakama ikamtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia chini ya vifungu namba 195 na 198 vya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16.

Mahakama ilibainisha kuwa marehemu alipata majeraha makubwa mwilini, ikiwemo kupasuka kichwa na kuganda kwa damu kwenye ubongo, hali iliyosababisha kifo chake. Aidha, ushahidi wa mazingira ulionyesha kuwa marehemu alionekana mara ya mwisho akiwa na mshtakiwa ndani ya gari lake aina ya Toyota Noah.

Ilielezwa pia kuwa baada ya tukio hilo, mshtakiwa alikimbilia Moshi akidaiwa kufanya hivyo kwa lengo la kupoteza ushahidi, kabla ya kukamatwa na kurejeshwa Iringa kwa ajili ya uchunguzi na hatua za kisheria. Mahakama ilibaini pia kuwa hakukuwa na kumbukumbu yoyote ya mtuhumiwa katika daftari la mahabusu (detention register) katika Kituo cha Polisi Ipogoro.

Katika utetezi wake, wakili Cleofas Mheluka aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu mshtakiwa, akieleza kuwa ni baba wa watoto watano, ana matatizo ya kiafya ikiwemo shinikizo la damu (BP) na maumivu ya mgongo, na kwamba hiyo ni mara yake ya kwanza kukabiliwa na kosa la jinai. Pia alidai kuwa tukio hilo halikuwa la kukusudia.


Kwa upande wa familia ya marehemu, baba wa marehemu, Lusiani Kiyeyeu, alisema hajaridhishwa na hukumu hiyo, akidai kuwa adhabu iliyotolewa ni ndogo ukilinganisha na uzito wa tukio, na kuiomba serikali kuingilia kati ili haki itendeke kikamilifu.

Hukumu hiyo imeibua mjadala miongoni mwa wananchi, baadhi wakidai adhabu hiyo ni ndogo, huku wengine wakisema ni fundisho kwa watumishi wa umma kuhusu umuhimu wa kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu yao.

Historia ya Tukio

Awali, Desemba 15, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Sajenti Rogers alipokea taarifa kutoka kwa mwananchi aliyemtuhumu Kiyeyeu kuiba simu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, askari huyo kwa kushirikiana na mgambo walimkamata mtuhumiwa na kumpiga, hali iliyosababisha kupoteza fahamu. Baadaye walimpeleka katika hospitali binafsi na kisha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, ambako ilibainika kuwa tayari amefariki dunia.

Kamanda Bukumbi alisema baada ya tukio hilo, watuhumiwa walitoweka na kuanza kusakwa na jeshi la polisi, huku akitoa wito kwa yeyote mwenye taarifa kusaidia ili sheria ichukue mkondo wake.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...