Skip to main content

MAMBO YA NDOA HAYOOOOOOO


Na Friday Simbaya


MSEMAJI Mkuu wa shirika  la TECONAREMAP Bw, Ochieng Anudo amesema kuwa Idara ya uchunguzi na upelelezi ya shirika hilo imefanikiwa kugundwa udanganyifu ya cheti feki cha ndoa ambacho Bi, Mwanaidi Musa alitumia kudai kuwa alifunga ndoa na Bw, Hussein Dodo.

Mali anazodaiwa kulipwa Bi, Mwanaidi kwa kutmia cheti feki hicho cha ndoa akidai ametelekezwa ni mashamba hekari 4, ng'ombe 30, mbuzi saba, kuku 20, bata 30 meza moja, mapipa ya ujazo manne pamoja na vyombo vingine vya ndani na kumwacha Bw, Hussein Dodo akiwa masikini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake mjini Iringa Bw, Ochieng alisema ofisi yake ilipokea malalamiko ya kuhujumiwa kwa haki za mazingira mtu kutoka kwa Bw, Hussein Dodo ambaye ni mkazi wa wilaya ya Babati akidai kuwa Bi, Mwanaidi Musa hakuwa mke wake na kuwa cheti cha ndoa alichotumia hakikuwa halali.

Alisema kuwa baada ya taarifa hizo idara yake ya uchunguzi na upelelezi wa shirika hili ilifanya uchunguzi wa kina ambapo walibaini cheti hicho hakikuwa halali ambapo njama zilitumiwa kwa kupitia cheti bandia hicho ili Bi, Mwanaidi ajipatie mali za kiuhujumu alizokuwa nazo Bw, Hussein Dodo.

Alisema kuwa walipokea pia barua kutoka kwa Katibu wa Baraza la Usuluhishi la BAKWATA la wilaya ya Babati iliyosainiwa na Bw, Abdi Isuja yenye kumbukumbu namba BKT/BBC/BU/2/20 ya tarehe 23 June 2010 ambayo inamtaka Bw, Hussein Dodo amfikishe kwenye mkono wa sheria kutokana na kutumia cheti feki cha ndoa ili kujipatia mali za udanganyifu kwa kudai kuwa amemtelekeza muda mrefu.

"Hivyo kwa hati hiyo ilivyo inaonesha udanganyifu umefanyika kwa Bi, Mwanaidi kutumia cheti feki cha ndoa kuihadaa BAKWATA ili alipwe mali wakati hakuwa mwanandoa na kwa kuwa Mzee Dodo ameadhirika katika mazingira mtu anatakiwa kufikishwa mbele ya sheria ili Bi, Mwanaidi arudishe mali na fidia zote alizosababisha", ilieleza sehemu ya barua hiyo.

Bw,  Ochieng alisema kuwa awali bw, Hussein Dodo alifika kwenye ofisi za TECONAREMAP na kwa kuwa shirika lake linafanya kazi mwa msaada wa sheria, ili aweze kusaidiwa kuzipata haki zake ambazo amepokonywa kwa njama na mwanamke huyo.

Aliongeza kuwa shirika hilo linatoa msaada wa sheria ili kuwasaidia watu waliopoetza haki zao kwa kuhujumiwa kupata haki  zao ambao wamehujumiwa na kuweza kuzipata na kuongeza kuwa ndipo kamati yake ya uchunguzi na upelelezi ilipofanya kazi kwa kushirikiana na BAKWATA wilaya ya Babati hadi kubaini udanganyifu huo.

Akizungumzia swala hilo kwa njia ya simu Katibu wa Baraza la Usuluhishi la BAKWATA la wilaya ya Babati Bw, Abdi Isuja alikiri kupokea kesi ya Bi Mwanaidi Musa akidai kutelekezwa na Bw, Hussein Dodo ambayo ilisababisha kufikiwa maamuzi ya kuchukuliwa mali isivyo halali.

"Amekiri na kusaini mbele ya baraza letu kimaandishi katika barua yake ya tarehe 5 June 2010 kuwa ameihadaa baraza kwa kuonesha cheti ambacho siyo sahihi, na kutokana na barua hiyo baraza la BAKWATA tumemwandikia Bw, Dodo aende kwenye vyombo vya sheria ili haki zake alizohujumiwa arejeshewe", alisema Katibu Abdi Isuja.

Bw, Isuja alisema kuwa baada ya kutumia cheti hicho feki Bi, Mwanaidi alichukua mali kutoka kwa Bw, Dodo zikiwemo ng'ombe 30, shamba ekari Nne, mapipa manne, mbuzi saba, kuku 20, bata 30 pamoja na vyombo vingine vya ndani amesema kuwa maamuzi hayo yalikuwa siyo sahihi, hivyo Bw, Hussein Dodo ameshauriwa kwenda kwenye vyombo vya sheria ili azipate haki zake.

Aidha Afisa wa TECONAREMAP NA MSAADA WA SHERIA  Bw, Ochieng Anudo ametoa wito kwa watu ambao wanahujumiwa haki zao kuyatumia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi kwa msaada wa sheria ambayo yatawasaidia kutafiti hadi waweze kuzipata haki zao

Aliongeza kuwa kwa kuwa Bi, Mwanaidi amemvunjia haki za kibinadamu na kukiri mbele ya baraza lake na shirika hilo baada ya uchunguzi walioufanya hatua za kisheria zinatakiwa zichukuliwe juu yake ili kuondoa malalamiko ambayo serikali inatupiwa kuwa haifanyi kazi wakati watu wanatumia mbinu zao kuhadaa ili kujinufaisha.
Bi Mwanaidi Musa alipohojiwa alikiri kuihadaa  kuwa niliihadaa baraza la BAKWATA kuwa ni hati ya kiisilamu kwa kuwapelekea cheti ambacho nilighushi na kuonesha kuwa alifunga ndoa na Bw, Hussein Dodo 22 Februari 1968 wakati siyo kweli.

“Nakiri kuwa cheti hiki cha ndoa siyo sahihi nilighushi ili nipate mali za Bw, Dodo, pia nakiri nililihadaa baraza hilo kwa hati hiyo ya ndoa kuwa ilitolewa na ni ya kiisilamu wakati siyo kweli”, alisema Bi, Mwanaidi na kuongeza kuwa alifikia maamuzi ya kutumia mbinu hizo baada ya Bw, Hussein Dodo kutompa haki zake pamoja na watoto wake ambao alizaa naye.

Aidha Bi, Mwanaidi alisema kuwa awali walikuwa wameoana na Bw, Dodo lakini walitengana baada ya kupewa taraka kisheria 1968 ila alitumia mbinu hizo ili apate mali kutokana na wakati akipatiwa talaka hakuweza kuzipata, alisema Bi Mwanaidi Musa

Ameliomba baraza la BAKWATA limsaidie ili apate haki hizo ili aweze kuwatunza  watoto wake ambao alizaa na Bw, Hussein Dodo na kuongeza kuwa watoto hao kwa sasa hawana msaada wowote ndiyo maana alifikia maamuzi hayo.


Akizungumza leo kwa simu  Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara RPC Parmena Sumari alipohojiwa alikiri kupokea barua katika ofisi yake ya madai ya Bi Mwanaidi Musa kutumia cheti cha ndoa cha kughushi na kujipatia mali isivyo halali na kuongeza kuwa ni mapema mno kulizungumzia lakini uchunguzi utafanyika ili kubaini ukweli wa jambo hilo.

"Ni kweli tumepokea barua yake inayodai Bi Mwanaidi hivyo polisi watafanya uchunguzi wa kina na kwa kuwa kughushi cheti ni kosa la jinai endapo Bi, Mwanaidi atapatikana na hatia hiyo atafikishwa mbele ya mkono wa sheria", alisema Kamanda Sumari.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...