Skip to main content

MWENGE WAINGIA MKOANI IRINGA

Na. Friday Simbaya,
Ludewa

JUMLA ya miradi sabini na moja (71) yenye thamani ya shilingi 8,369,893,729 itakaguliwa, kuzinduliwa, itafunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi mkoani Iringa kwa mwaka 2010 wakati wa mbio za mwenge.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu tawala mkoa wa Iringa Bibi. Gertrude Mpaka juzi wakati akisoma taarifa fupi ya mkoa wa Iringa wakati wa kupokea mwenge wa uhuru mwaka 2010 katika kijiji cha Kipingu, kata ya Manda wilayani Ludewa ukitokea mkoani Ruvuma.

Bi.Mpaka alisema miongoni mwa fedha hizo, shilingi 2,890,484,593 ni fedha toka Serikali kuu, shilingi 951,705,586 ni michango ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa, thamani ya nguvu kazi ya wananchi ni shilingi 1,557,402,245, shilingi 1,413,904,000 ni michango ya watu binafsi na shilingi 1,556,397,305 ni michango ya wahisani na taasisi mbalimbali za maendeleo .

Mwenge wa uhuru mwaka huu unaongozwa na ujumbe usemao “Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na Malaria”

Katibu tawala mkoa alielezia kuwa mapambano dhidi ya Ukimwi yanaendelea kwa kasi mkoani Iringa, na mkoa kwa kushirikiana na asasi za kitaifa na kimataifa na tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) umetekeleza mpango maalumu wa miaka minne wa kupambana na tatizo la Ukimwi ambapo utekelezaji wake ulianza Oktoba, 2008 na utamalizika Septemba 2012 .

Ameyataja maeneo makuu kuwa ni; kuhakikisha upatikanaji wa kutosha na kuendelea kutoa elimu ya juu ya matumizi sahihi ya kondomu, kupeleka karibu na kuboresha huduma za afya kwa jamii ambapo katika kipindi cha 2008/ 2009 jumla ya vituo 35 vya kupima virisi vya Ukimwi na kuto ushauri nasaha (CTC) vimeboreshwa kwa kufanyiwa ukarabati na samani.

Aidha wataalam 227 wamepatiwa mafunzo rejea kuhusu virusi vya Ukimwi na ushauri nasaha na jumla ya wagonjwa 51,137 walifikiwa na huduma za kupima virusi vya Ukimwi na kupata ushauri nasaha (CTC).

Eneo jingine amelitaja kuwa ni kuzijengea uwezo jamii wa kupambana na mila na desturi hatarishi zinazochangia ongezeko la maambukizi mapya ya VVU. Pia kuboresha huduma za magonjwa ya zinaa ambapo katika kipindi cha mwaka 2008/ 2009 kulikuwa na jumla ya vituo 293 vinavyotoa huduma ya magonjwa ya zinaa, wataalamu 288 walipatiwa mafunzo rejea ya huduma za matibabu ya magonjwa ya zinaa na watu 7,569 walifikiwa matibabu ya magonjwa ya zinaa.

Bibi. Mpaka ameongeza eneo lingine kuwa ni kuongeza elimu na uhamasishaji juu ya masuala ya ngono salama kwa makundi yaliyo katika mazingira atarishi ambapo katika kipindi cha mwaka 2008/2009 jumla ya mikutano 395 ya uhamasishaji katika ngazi mbalimbali za jamii ilifanyika, aidha vikundi 181 vya kijamii vilishiriki na jumla ya vipeperushi na mabango 23,000 vya kuelimisha jamii.

Wakati huohuo katika mbio zake zilizoanza wilayani Ludewa jana Mwenge wa uhuru umekagua umekagua, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya msingi jumla ya miradi 13 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...