Skip to main content

LUDEWA WAGOMA KUWAPOKEA WATANZANIA WAPYA


WANANCHI katika Wilaya ya Ludewa Mkoani Iringa, wamekataa katu kuwapokea wakimbizi kutoka Somalia na Ethiopia waliobatizwa kwa jina la watanzania wapya kwa madai kuwa watasababisha hasara kubwa kuliko faida imefahamika.

Mgomo huo umetokea jana katika kikao cha Baraza  la Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi kilichofanyika Julai 15 mwaka huu ambacho pamoja na mambo mengine kilihusisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa miradi  ya maendeleo kwa mwaka wa fedha uliopita.

Awali akitoa taarifa ya kutaka ufafanuzi Diwani wa Kata ya Mawengi, Bw. Leodgar Mpambalyoto alisema kuna jambo lililoko mbele yetu linalowasumbua wananchi wengi ambalo ni agizo la serikali la kuwapokea watanzania wapya ambao wamebatizwa jina hilo kutokana na kuingia nchini na kupokelewa kama wakimbizi.

Kwa upande, wake Mpambalyoto aliishauri serikali kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na baadhi ya wadau wakiwemo madiwani. “Ni wajibu wa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri kupokea maelekezo kutoka Serikali Kuu, lakini baraza lina uwezo wa kukataa au kukubali kwani ndiyo wawakilishi wa wananchi,” zoezi la kuwapokea watanzania wapya bila maelekezo litakuwa na athari kubwa sana tunaomba lisipuuzwe,” aliongeza.

Akichangia hoja hiyo Mbunge wa Ludewa Bw. Deogratius Haule Filikunjombe alisema kuwa waraka huu ulishasainiwa na rais tayari na ulishapitishwa, lakini ukiangalia zaidi watu hawa wakija wanamadhara zaidi kuliko faida.

“Pamoja na kwamba rais ameridhia mila za watu hawa na zetu hazifanani, wanakotoka ni watu wa vita, leo hii Ludewa tunaletewa watu elfu tatu je, wana Ludewa wameandaliwa?  Sisi tupo tayari?  Kama sehemu nyingine wanawahitaji, sisi Ludewa hatuwataki,”alisisitiza mbunge huyo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Bi. Hilda Lauwo aliwaambia madiwani hao kuwa anataarifa kuwa wahusika walisema wangekuja kutoa mafunzo hayo ili kupata uelewa aliwataka wasikatae mafunzo hayo na kwamba wayapate kwanza ndipo wayakatae.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria baraza hilo walishtushwa na hatua ya serikali kuleta wageni nyumbani kwao bila kuwashirikisha na kukubaliana, walisema pamoja na kwamba waraka huu umetoka kwa mkuu wa nchi ambaye ni Rais Jakaya Kikwete, siyo vizuri kuwaleta watu hawa wanaotoka kwenye vita katika maeneo yetu hatuwezi kujua wamekuja na nini.

“Sisi wenyewe hatuna sehemu ya kulima tunahangaika kwa umaskini sasa hawa watanzania wapya wanaotaka kuja katika miji yetu, kwani huko kwao walikotoka hawawezi kurudishwa?” waliuliza wajumbe hao kwa maskitiko.

 Taarifa hiyo ya utengamanishaji wa mkakati wa kufungua makazi mapya na kuwezesha ukaaji wa watanzania wapya waliopewa uraia katika maeneo tofauti nchini,  inasema serikali ya Tanzania kuwezesha uhamiaji wa makazi ya kaya za Watanzania wapya waliopewa uraia zipatazo 35,500 kutoka katika makazi ya wakimbizi.

Katika zoezi hilo serikali imeteua wilaya zaidi ya 50 kutoka mikoa 16 ambayo ni pamoja na Iringa kaya
3,000, Rukwa 3,000, Dodoma 3,500, Ruvuma 3,000, Shinyanga 1,600, Morogoro 1,600, Tabora 1,600, Tanga 1,600, Kigoma 1,000, Singida 1,600, Pwani 2,000, Mtwara 3,500, Mbeya 1,500, Manyara 1,500, Lindi 3,500, na Kagera 1,500 vigezo vilivyotumika katika uteuzi wa mikoa hiyo ni upatikanaji wa ardhi ya kulima na hali ya msongamano wa watu.

Wilaya ya Ludewa inazo tarafa tano, kata ishirini na tano na vijiji sabini na sita wakazi wake wako laki moja na nusu kwa mujibu wa Sense ya Mwaka 2000. Ludewa inavivutio vingi ikiwemo milima ya Livingstone, samaki wa mapambo Ziwa Nyasa, madini aina nyingi tofauti.
                  

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...