Skip to main content

MHANDISI AKESHA ENEO LA MRADI WA MAJI

MHANDISI  WA MAJI LUDEWA ASHANGAZA KWA KUACHA FAMILIA NA KUKESHA ENEO LA MRADI KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA MAJI SALAMA NA KWA WAKATI.
          
WANANCHI katika Kata za Manda, Luilo na Masasi katika Tarafa ya Masasi Ludewa, mkoani Iringa wameiomba serikali kuongeza nguvu zaidi katika mradi wa maji uliokuwa umeshindikana muda mrefu ama kwa kukosa rasilimali wataalamu wenye uwezo au fedha ili kuweza kufikisha maji katika maeneo yaliyobaki baada ya Bw. Christopher Nyandiga (Mhandisi wa Maji wilayani humo) kufauru kufikisha maji katika baadhi ya maeneo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau, wananchi na watumiaji wa maji hayo hawakusita kumshukuru na kumpongeza mhandisi wa maji wilayani humo Bw. Christopher Nyandiga na kumtaja kama mkombozi wa maisha yao kwa kuwa ni miaka mingi maji ya bomba yamekuwa ndoto kwao kutokana na ukilitimba wa wataalam na wahandisi waliotangulia.
“Mradi wa maji katika Tarafa yetu ya Masasi una historia ya ajabu kuna wakati katika miaka ya themanini, Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi aliitwa kuja kuzindua tanki la maji kumdanganya kuwa maji hayo yametokana na bomba kumbe waliyachota ziwa nyasa na kuyajaza na baada ya kuzindua tu ukawa ndiyo mwisho,” alisema mmoja kwa masharti ya kutoandikwa jina gazetini.
Alisema wananchi wana kila sababu ya kuishukuru Halmashauri ya Wilaya kwa kusikia kilio chao, lakini pia kwa kuwapelekea mhandisi mbunifu, mwenye uwezo kitaaluma, lakini mwenye kujituma kwani hawajawahi kuona mtaalam kuacha familia yake na kuhamia katika eneo la mradi huku yeye mwenyewe akifanya kazi kama fundi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Matei Felician Kongo akizungumza katika eneo la mradi alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Hilda Lauo kwa uwamuzi alioufanya hasa Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ludewa Bw. Christopher Ndindiga kwa kuvua cheo chake na kuhamia eneo la mradi hadi ulipokamilika.
“Mradi huu si wa leo ni wa muda mrefu sasa ni zaidi ya miaka ishirini,  awali ulikuwa ukiitwa Lifua- Manda Project wakati huo kulikuwa na ugonjwa wa kipindupindu huku ukilenga kupeleka maji hayo katika Sekondari ya Manda,” alisema Bw. Kongo huku akifurahia mafanikio.
Bw. Kongo alisema katika miaka ya 1979 hadi 1980 mradi huo ulikuwa unategemea chanzo cha mto Kilumbila ambao sasa unaendeshwa na wamisionari, hata hivyo hakuwa na uhakika kama ni shilingi ngapi zilitumika katika miradi hiyo kwani ni muda mrefu sasa.
Mradi huu mpya chanzo chake ni mto Mchuchuma ambao unayomaji ya kutosha na unahudumia kwa sasa katika vijiji vya Luilo, Lihagule, Manda na Masasi, hata hivyo mradi wenyewe umekuwa wa kuungaunga hii ni kutokana na fedha kutofika kwa wakati na wakati mwingine kuwa kidogo.
Bi. Winfrida Kilumbo (Kizota) Diwani wa Kata ya Manda kwa upande wake alimshukuru na kumpongeza Mhandisi wa Maji, Bw. Christopher Nyandiga kwa moyo wa kizalendo kwani aligeuka kuwa fundi yeye mwenyewe na kuuweka uhandisi pembeni.
Kizota alisema Wananchi wa Manda wamekuwa wakitumia maji ya Ziwa Nyasa ambayo kwa kipindi cha masika si salama. Lakini mradi huu ni ukombozi mkubwa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Manda na walimu kwani wamekuwa wakitegemea maji ya ziwa yanayopatikana umbali wa zaidi ya kilomita tano.
“Wanafunzi wamekuwa wakibeba maji kichwani kwa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na walimu wao kila siku wanapokwenda shuleni kwa kipindi chote cha miaka mine, lakini tunashukuru sasa tatizo hili limekwisha baada ya maji kufika shuleni hata ujenzi wa majengo umerahisishwa,” alisema Bi. Kizota.
Kwa upande wake, mhandisi wa maji wilayani Ludewa Bw. Nyandiga alisema alilazimika kufanya hivyo kutokana na shida wanayoipata wananchi wa Tarafa ya Masasi kwa muda mrefu sasa na kwamba amefanikiwa kuyafikisha maji katika baadhi ya maeneo machache na kwamba sehemu zingine zitaendelea kupata kadri ya upatikanaji wa fedha, lakini akawataka wananchi kutunza na kuyalinda mabomba hayo ili yaweze kuwatunza.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...