Skip to main content

DC LUDEWA ACHANGISHA MILIONI 5 ZA UJENZI WA SHULE NA KUSEMA LUDEWA WAGUMU KUCHANGIA ELIMU WEPESI KWENYE SHEREHE.

MKAMATE elimu usimwache aende zake maana yeye ni uzima wako, na kama unadhani elimu ni gharama basi, jaribu ujinga. Hiyo ni kauli mbiu iliyotumika jana katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Sekondari ya Matakatifu Alois inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, Parokia ya Ludewa.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi. Georgina Bundala kama mgeni rasmi akiwakilishwa na Afisa Maaendeleo ya Jamii Wilaya Bw. Lazaro Mapunda aliongoza harambee hiyo iliyohudhuriwa na wadau na wananchi wachache lakini akafanikiwa kuchangisha jumla na zaidi ya shilingi 5m/- na kuungwa mkono na wageni kutoka makao makuu ya Jimbo Katoliki la Njombe.

Wananchi wilayani Ludewa wanatakiwa kushiriki na kuwekeza zaidi katika elimu ili kuongeza idadi ya wataalamu wilayani humo na Taifa kwa ujumla badala ya kupoteza muda na fedha nyingi kwenye vikao vya harusi na sherehe zingine zinazohusiana na mambo ya burudani,kuselebuka, kulakula na kunywa huku watoto wakiendelea kufanya vibaya katika mitihani yao.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi Georgina Bundala kwenye Ukumbi wa Kanisa Katoliki la Yesu Kristo Mkombozi Parokia ya Ludewa katika harambee maalumu ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Mtakatifu Alois inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Mdonga nje kidogo ya Mji wa Ludewa.

Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Paroko wa Parokia ya Ludewa Fr. Ladislaus Mgaya alisema kuanzishwa kwa shule za msingi na sekondari zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki, Jimbo la Njombe kunatokana na tamko la Askofu wa Jimbo Alfred Maluma la mwaka 2003, lilinukuliwa kwenye Kitabu cha Mithali Sura  ya 22 aya ya sita inayosema (mlee mtoto katika njia ipasayo naye hataiacha hata akiwa mzee).

Fr. Ladislaus Mgaya alisema Elimu na Malezi bora. Huu ndio wimbo tutakao kuwa tunaimba na kugharamia elimu, tamko hili lilianza kutekelezwa mwaka 2004 na Ludewa likaanza kuzaa matunda mwaka 2007 ambapo majengo yalianza kujengwa kwa nguvu za waumini wenyewe.

Fr. Mgaya alizitaja Changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na ujenzi wa maabara na nyumba tatu za walimu vyote vikiwa na thamani ya shilingi 50m/- na kwamba kwa sasa idadi ya wanafunzi shuleni hapo ni 98 wakiwemo wasichana 35 tu.

Naye Mkurugenzi wa elimu katika Jimbo Katoliki la Njombe, Fr. Bruno Henjewele aliwataka waumini na wananchi wote wa Ludewa kutofanya uzembe katika suala la elimu kwani badaye wanaweza kuja kupata majuto yenye maumivu makali kwani dunia ya leo bila elimu ni aibu kwa sababu hata vibarua wa kufagia atatakiwa kuwa na vyeti vya sekondari.

Wageni waliomwakilisha Baba Askofu katika Harambee hiyo ni pamoja na Fr Alexanda Mlelwa ambaye ni Paroko wa Parokia ya Makete na Mwenyekiti wa Mapadre wazawa Jimbo la Njombe, Fr Bruno Henjewele Mkurugenzi wa Elimu Jimbo, Mkuu wa Shule ya Msingi SICRED waliochangia shilingi laki tano, Shule ya Msingi Bakita waliochangia laki mbili na nusu.

Wengine Mkuu wa Shule ya Sekondri ya Ilowola waliochngia shilingi laki nne, Masista wa shule ya Mtakatifu Monica Seminari ya wasichana walichangia shilingi laki mbili, Shule ya Sekondari wavulana (Umawanjo) inayotegemea kujengwa Upangwa Bonde la Ludewa Lugarawa chini ya umoja wa mapadre nayo ilitoa shilingi laki moja sitini elfu taslimu.

Jimbo Katoliki la Njombe hadi sasa limefanikiwa kujenga shule nyingi zikiwemo za msingi na sekondari.

Mji wa Ludewa Pamoja na kuwa na makanisa Lukuki yanayoibukia kila kukicha kwa kuhubiri neno la Mungu ni Kanisa moja tu la Kianglikana ndilo lililoshiriki vyema harambee hiyo kwa moyo na kuchangia shilingi laki moja chini ya Mchungaji wake Padre Mtweve ambaye kwa upande wake aliwasihi wachungaji wenzake, na wananchi kwa ujumla kuwa waache kushiriki kwenye mialiko yenye kula waache tofauti za imani na kushiriki katika mambo ya msingi kama elimu kwani hata maandiko matakatifu yanaelekeza hivyo.

Elimu ni Sarakasi na kujenga shule moja ni sawa na kujenga makanisa mengi.Hiyo ilikuwa  kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya walei Parokia ya Ludewa Bw. Linus Njalla Ngalomba alipokuwa akihitimisha harambee hiyo kwa kuwashukuru wale wote waliofanikisha zoezi hilo sambamba na wageini kutoka Jimboni Njombe.

                          

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...