Skip to main content

ZAHANATI YA KILONDO NA LIFUMA ZAPATA WAGANGA WASTAAFU NI BAADA YA MBUNGE KULIPA POSHO TOKA MFUKONI MWAKE


.

WANANCHI katika Kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Iringa  wamepata furaha iliyopindukia na baadae kuikataa Boti iliyopelekwa na Mbunge wao   Deo Filikunjombe kama ‘Ambulance’ kwa ajili ya wagonjwa baada ya mbunge huyo kuwapelekea tena mganga katika zahanati yao.
Kilio cha muda mrefu kwa Wananchi wa Kilondo ni mganga ndiyo maana mbunge wao alipowapelekea mganga na boti kwa wakati mmoja walichagua mganga na kusema hakuna haja ya boti kwa sababu waliomba boti ili kuwasafirisha wagonjwa kuwapeleka kwa mganga.
Uamuzi wa mbunge huyo kuamua kutoa fedha yake ya mfukoni na kuwalipa posho waganga wastaafu ulikuja baada ya Halmashauri ya Wilaya kushindwa kupeleka waganga katika zahanati hizo huku wananchi wakipoteza maisha kwa magonjwa ya kawaida.
Akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni Bw. Filikunjombe alisema kuwa wananchi wa Kilondo ni binadamu kama walivyo wengine, lakini wanakosa huduma muhimu pengine kutokana na mazingira magumu ya Kata  na wilaya nzima  .
Alisema kuwa kuna haja ya kuweka mkakati wa kudumu hasa kwa kuwasomesha vijana wa kutoka mazingira yale na kuingia nao mkataba shida itakwisha.akaongeza kuwa kote kuna mazingira magumu, lakini Kilondo kuna mazingira magumu zaidi kuliko Ibumi.
Mkakati huu ni vema uanze sasa lakini pia kwa kuwa mmeridhia kuwa wapelekwe waganga wastaafu kwa muda kutokana na kukosekana kwa waganga niko tayari kuchangia wakati Halmashauri inafanya mkakati wa kudumu kupata waganga katika zahanati ya Kilondo na Lifuma. alisema mbunge huyo.
Habari kutoka ndani ya ofisi ya utumishi zinasema watumishi hao wastaafu ambao ni Martha Ngalawa (Lifuma) na Philipo Kayombo Mbufu (Kilondo) watalipwa posho kulingana na mshahara waliokuwa wakipata kabla ya kustaafu kwao.
Mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani kushiriana na watendaji wa Halmashauri kuliko kuwindana kwani kufanya hivyo kutadhoofisha maendeleo ya wananchi, akahimiza kufanyakazi kama timu kwa upendo kwa sababu lengo ni moja.
Bw Deo aliwaagiza viongozi, watendaji na bodi ya zabuni kuangalia na kutoa kipaumbele kwa kuwapa kazi makandarasi wa ndani wazalendo wenye uwezo ili kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya halmashauri kuliko kutoa tenda zote kwa wageni ambao baada ya kumaliza huondoka na fedha nje ya wilaya.
Akiwakilisha hoja kwa niaba ya baraza, Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Masasi Bi Lucy Haule alisema  kuwa madiwani wa Ludewa wanakuwa wakiimba wimbo mmoja akimaanisha kuwa kutokana na shida inayowakabili wananchi wa mwambao na  kuwa Halmashauri imepata magari mawili ya wagonjwa ni vema na haki moja liende mwambao.
“Kutokana na shida iliyopo Kata ya Lupingu hasa inayowakabili wagonjwa na wajawazito baraza lako tukufu linaaigiza kwamba gari moja la wagonjwa lipelekwe katika kituo cha Lupingu kupunguza tatizo,” alisisitiza Bi. Lucy.
Baada ya kutoa agizo madiwani wote kwa kauli moja waungamkono hoja na kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Bi Hilda Lauo kutekeleza agiza hilo bila kuchelewa na tayari gari hilo limeshapelekwa Lupingu.
 Filikunjombe aliwashukuru madiwani kwa kuridhia kwa upendo na utayari wa kuruhusu gari la wagonjwa kwenda kusaidia mwambao wa Ziwa Nyasa badala ya Mlangali, lakini aliahidi kulisimamia na kulifuatilia gari la Mlangali ili liweze kufika haraka.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...