Skip to main content

MADEREVA WAASWA KUZINGATIA ALAMA ZA BARABARANI


Na Vicky Macha,
Iringa.

MADEREVA wanatakiwa kuzingatia alama za barabarani ili kukabiliana na ajali za mara kwa mara  hasa zinazojitokeza katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TANZAM).

Rai hiyo ilitolewa jana na Mkandarasi wa Mradi wa ujenzi wa barabara kutoka makao makuu (Tanroads) Kenfas Mahenge wakati wa makabidhiano rasmi ya barabara hiyo na  makandarasi wa kampuni ya Aarsleff- Interbeton Denmark mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa barabara hiyo mwishoni mwa wiki.

Mahenge alisema hali ya nchi ilivyo ambayo ni ya milima, miteremko na kona nyingi hasa katika maeneo ya hifadhi ya wanyamaMikumi ni lazima kila dereva kuzingatia alama hizo pindi apitapo katika barabara hiyo kwani kumekuwa na ongezeko la ajali zinazoendelea kuwatafuna wananchi hasa abiria.

Alisema kwa kuliona hilo walilazimika kumtaka mkadarasi kuweka kila eneo alama ikiwemo matuta, lakini kumeoneka  madereva kuendesha magari kwa uzoefu mbali na kupatiwa elimu ya udereva.

Hata hivyo alisema  utaratibu wa kuwatoza fidia waharibifu wa barabara pindi ajili inapotokea ni pamoja na  kukamata bima zao ikiwa ni harakati za kutokomeza ajali zisizo za lazima.

Naye Meneja wa wakala wa barabara wa mkoa wa Morogoro (Tanroads) Charles Madinda alisema kumekuwa na uzembe kwa baadhi ya madereva hasa nyakati za usiku na husababisha ajali nyingi na wakati mwingine ajali hizo huwa ni za uzembe ikiwemo mwendo kasi.

Alisema sheria ya mwaka 2007/ 2009 kifungu cha 13 ya kulipa fidia endapo ajali itatokea na kuharibu barabara na alama zilizowekwa inafuatwa bila ya kumtazama ni mtu wa nafasi gani katika nchi kwani gharama za ujenzi ni mkubwa hivyo ni lazima kuzingatia muda ulioweka kwa matumizi ya barabara hiyo.

“ Barabara hii ni lazima itunzwa kwa madereva na hata wananchi waishio jirani na eneo lililopita barabara ili iweze kudumu kwa miaka zaidi ya 20 kama ambavyo imekusudiwa na ni wajibu wa kila mmoja,” alisema.

Kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara mkaoni Iringa (Tanroads) Paul Lyakurwa alisema wakandarasi hao wamejenga barabara hiyo kwa fedha ambzo walitakiwa kuzitumia bila ya kupungua wala kuzidisha.

Alisema barabara ambayo wameitekeleza inaukubwa wa kilometa 150 ambayo ilikuwa na sehemu nne ambazo ni Iyovi – Ruaha Mbuyuni km 40, Ruaha Mbuyuni – Kitonga km 47, Ikokoto – Iringa km 61 na Iringa Mjini km 2 iliyojengwa kwa fedha za US$ 110 milion  / Euro 76.2 Milion.

Lyakurwa alisema kutokana na hali ya uwaminifu wao kwa kuzingatia muda na kiasi cha fedha za makubaliana wamelazimika kuwapa sehemu nyingine ya ujenzi wa barabara itokayo Iringa - Mafinga  yenye urefu wa km 68  ambayo inatarajiwa kuanza rasmi mapema Septemba 18, 2011 na kumalizika July 9, 2013 kwa Euro 38.5m (us$ 46.2m).

Mradi huo wa awali ulianza rasmi September 19, 2008 kwa makubalina ya miaka mitatu ambayo ni 18 Sept 2011 na imemalizika kwa kuzingatia makubalina hayo.

Mwisho.
0713 654945






Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...