Skip to main content

"Tanga Fresh Ltd" yakumbwa na changamoto mbalimbai katika uzalishaji maziwa


Na Gustav Chahe, Tanga

Kiwanda cha uzalishashi maziwa “Tanga Fresh Limited” kilichopo Mkoani Tanga kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa zao la maziwa hali inayotokana na ukosefu wa malisho kwa ng’ombe hasa kipindi hiki cha kianzazi.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi kiwandani hapo hivi karibuni, afisa habari wa kiwanda hicho Bw. Charles Tumaini ameeleza kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinalazimika kujiendesha kwa hasara kutokana na kushindwa kufikia asilimia 100 ya uzalishaji kulingana na nguvu ya mitambo iliyopo.

“Kwa sasa uzalishaji ni asilimia 60 tu ambayo sawa na lita 50,000 tu kwa masaa 8, hatujafikia kiwango cha asilimia 100 ya uzalishaji kulingana na nguvu ya mitambo yetu; kwa sasa tunazalisha asilimia 60 tu ambayo sawa na lita 50,000 kwa muda wa masaa 8 kila siku” alisema Bw. Tumaini.

“Tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatukwamisha kuzalisha maziwa kwa wingi ambazo miongoni mwake ni kukosa malisho, maji ya kutosha na kukosa chakula cha kutosha kwa wanyama wetu” alisema Bw. Tumaini.

Mbali na kiwanda kukosa uwezo wa kusambaza chakula kwa wafugaji wao, baadhi ya wafugaji wenyewe wamekuwa wakishawishwa na bei za mitaani na kuuza maziwa yao huko na kiwanda kukosa maziwa yakutosha.

“Baadhi ya wafugaji wamekuwa wakishawishwa na bei za mitaani na kuuza maziwa yao huko huku kiwanda kikiwa kikikosa maziwa ya kutosha” alisema.

Lita moja ya maziwa kiwandani hapo hununuliwa kwa shilingi 528 wakati mitaani watu hununu kwa shilingi 1,000 mara mbili ya bei ya kiwandani.
Licha ya wafugaji wengi kuuza maziwa yao mitaani, wengi wao hawana mafunzo ya ufugaji na kushindwa kuzalisha maziwa yenye kiwango na kuiomba serikali kutoa mafunzo kwa wafugaji kupitia maofisa ugani waliopo pamoja na kuongeza idadi yao ili kuweza kuboresha ufuji.

“Wafugaji wengi wanakosa mafunzo na kushindwa kuzalisha maziwa yenye kiwango. Hivyo, tunaiomba serikali katika kilimo kwanza wawafikirie wafugaji ili nao wapewe kipaumbele hasa katika kuwapa mafunzo. Pia maofisa ugani waendelezwe na wapewe mafunzo ya kutosha ili waweze kuwahudumia wafugaji na kuboresha ufugaji wao” alisema.

Serikali imeombwa kuingilia ili kuwepo na mpango endelevu wa kupata maziwa mazuri yakutosha kwa ajili ya uzalishaji kiwandani hapo ikiwa  ni pamoja na kuweka mpango endelevu wa uthibiti wa magonja ya mifugo.

“Tunaiomba hata serikali iingilie ili tuweze kupata maziwa mazuri; wakati mwingine inatokana na kutokuwepo mpango maalumu wa uthibiti wa magonjwa ya wanyama. Hivyo, tunaomba uwepo mpango endelevu wa uthibiti wa magonjwa hayo ili uzalishaji wa maziwa uweze kuongezeka kila siku vinginevyo tutapoteza uzalishaji wetu na kipato” alisema.

Bw. Tumaini amewaomba wafugaji kutokukata tama katika kipindi hiki na kuendelea kupeleka maziwa kiwandani hapo bila kujali changamoto zinazojitokeza.

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...