Skip to main content

ASKOFU SIMALENGA AZUILIWA KUINGIA KANISANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA VIFAA VYA BILIONI MOJA (1BN/=), MTIKILA ASEMA YUKO TAYARI KUONESHA VILIPO.

Na Mwandishi Wetu, Ludewa


TUHUMA za ubadhilifu wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja zinazomkabili Askofu John Simalenga wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Southwest Tanganyika Njombe, umechukua sura mpya baada ya waumini wenye hasira kumzuia kuendesha Ibada Milo. Dhahama hiyo ilimpata mchungaji huyo wa kiroho Oktoba 23, 2011katika Kanisa la Kung’aa kwa Bwana lililoko Mtaa wa Milo wilayani Ludewa mkoani Iringa, alikokwenda kuendesha Ibada ya Kipaimara. Awali waumini hao walimsimamisha kazi mchungaji wa mtaa wa Milo Padre Jophrey Mturo na kumnyima mshahara kwa madai kuwa ameshiriki ubadhirifu huo ndiyo maana amekuwa akimtetea Askofu huyo. Hata hivyo, Padre Mturo alilazimika kufungasha mizigo yake siku hiyohiyo na kukimbilia Kijiji cha Mlangali kwa hofu ya kuvamiwa na waumini wenye hasira na kwamba anasubiri maelekezo ya Askofu kuhusu kupangiwa kituo kingine cha kazi. Wakizungumza kanisani hapo waumini na viongozi wa mtaa huo walisema wameamua kumzuia mlangoni Askofu Simalenga kutokana na dharau alizoonesha kwao kwa kukaidi kutoa maelezo kuhusu ni wapi amepeleka vifaa vya hospitali yao vilivyotoka Ujerumani mwanzoni mwa mwaka huu. Katika madai yao waumini wanadai Askofu Simalenga pamoja na wenzake, mwanzoni mwa mwaka huu walipokea kontena lililo sheheni vifaa vya hospitali yao na vifaa vingine vya utabibu zikiwemo kompyuta 154 vyote vikiwa na thamani ya shilingi bilioni moja (1bn/-). Michael Mwinuka ni Katibu wa Mtaa na mwalimu katika Kanisa la Kung’aa kwa Bwana Milo. Kwa upande wake alisema waumini wamechoshwa na ubabe wa Askofu Simalenga ndiyo maana wameungana na kumtaka afanye kikao kwanza ndipo aendeshe Ibada. Mwinuka amesema yapo mambo mawili yaliyo pelakea waumini kumzua Askofu kuingia kanisani ikiwemo kuja kutoa Kipaimara kwa watoto ambao hawamaliza mafundisho kwa mujibu wa taratibu za kanisa. “Watoto wanatakiwa kuhudhuria mafundisho kwa kipindi cha mwaka mzima, lakini wamemaliza miezi miwili tu jambo lililopelekea wazazi kuwazuia watoto wao wakidai kuwa wangepata kipaimara bila kukomaa kiimani,” alisikitika Mwinuka. Alisema idadi ya watoto waliokuwa wanahudhuria mafundisho ya kipaimara walikuwa 43 kwa muda wa miezi miwili, lakini baada ya wazazi kuwazuia watoto wao walibaki watoto 8 watatu wakiwa watoto wa padre. Akaongeza kuwa waumini wamechoshwa na uovu, ubabe, udharimu na tabia chafu za Askofu Simalenga kwani amefanya kanisa kama mali yake binafsi jambo ambalo linawatia kichefuchefu waumini na kwamba kama angeacha kiburi tusingefikia hatua hii. Askofu Simalenga alipata wakati mgumu na kulazimika kujificha ndani siku nzima hata Polisi wa Kituo cha Mlangali walipokwenda kutaka kujua kulikoni hakuwa tayari kujitokeza mbele ya viongozi na waumini wa kanisa hilo, akidai atapanga siku nyingine. Mchungaji Christopher Mtikila akizungumza kijijini hapo alikokwenda msibani alisema amefurahishwa na ujasiri wa waumini wa Milo kwani inaonesha wameanza kuzitambua haki zao na kuchoshwa na ufisadi wa kiongozi wao na kuwataka Watanzania kuiga hatua hiyo. Mimi niko tayari kutoa ushirikiano kwa kuonesha mahali zilikouzwa, kompyuta, X-Ray na vifaa vingine kwa sababu aliyenunua yupo anafahamika na anakubali kwanini kuwazungusha waumini kiasi hicho? aliuliza Mtikila Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Milo Ananias Mwinuka alikiri kutokea kwa mgogoro huo wa muda mrefu na kwamba siku ya tukio aliitwa na kuhudhuria kikao kati ya polisi, waumini na viongozi, lakini Askofu alikataa kuhudhuria jambo lililo shangaza wengi. Alimtaka Mchungaji huyo kumaliza mgogoro kwa njia ya mazungumzo siyo ubabe. Naye Msaidizi wa Askofu Vicar General Kenani Michael Mlelwa akizungumza kwa njia ya simu alithibitisha bosi wake kuzuiliwa kuendesha Ibada Jumapili ya Oktoba 23 mwaka huu, lakini akawataka waumini kuwa na subira. Alikiri kuwepo kwa malalamiko dhidi ya Askofu Simalenga kwa muda mrefu na kusema kuwa madai hayo siyo ya kweli na kuongeza kuwa Askofu atapanga kuonana na waumini hao siku nyingine watakapokuwa wamepunguza jazba. Mgogoro wa kumtuhumu Askofu Simalenga juu ya ubadhilifu wa vifaa vya kanisa ulianza kufukuta mwanzoni mwa mwaka huu na kila alipotakiwa kutoa ufafanuzi alikaidi maombi ya waumini wake.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...