Skip to main content

WAAJIRI AMBAO HAWAPELEKI MICHANGO YA WANACHAMA WATAWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA

Na Friday Simbaya
Afisa Mwandamizi wa Shughuli (Senior Operations Officer) wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma  Bw. Bernabers W. Ndunguru ametoa wito
Baadhi ya wafanyakazi wa Abasia ya Peramiho wakipitia vipeperushi mbalimbali waktati semina  ilioendeshwa na maafisa kutoka Mfuko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  mkoa wa Ruvuma. 


Mwakilishi  wa  mwajiri  wa Abasia ya Peramho,  Bw. Kelvin Zenda akiwatambulisha maafisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)  mkoa wa Ruvuma kwa wanachama ambao ni wafanyakazi wa Abasia ya Peramiho wakati wa semina  katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Peramiho. Kutoka kulia kwake ni Bw. Barnabers W. Ndunguru (Senior Operations Officer NSSF Ruvuma), kushoto kwake  ni Bw. Mussa  Adam (Compliance Officer NSSR Songea) akifuatiwa na Bw. Michael William (Compliance Officer, Songea). (Picha na Friday Simbaya)

kwa waajiri ambao hawapeleki michango ya wanachama kwamba  watawachukulia hatua za kisheria wakibainika.
Afisa huyo mwandamizi alitoa rai wakati semina kwa wanachama ambao ni wafanyakazi wa Abasia ya Peramiho, Songea mkoani Ruvuma  kuhusu huduma mbalimbali zinazotoliwa na mfuko huo, iliofanyika tarehe 05.10.2013 katika Ukumbi wa Trade School.
 Alisema kuwa mwajiri anawajibu kisheria kujiandikisha kuwa mwajiri mchangiaji na kuandikisha wafanyakazi kwa kupeleka michango ya wanachama kila mwezi.
Aliongeza kuwa  mwajiri atafanya makato ya asilimia 10 ya jumla ya mapato yote ya mfanyakazi wake kwa  mwezi na naye kama mwajiri kuchangia asilimia 10, sawa na mapato ya mfanyakazi huyo n na kuwakilisha jumla ya makato hayo 20% kila mwezi kwenye shirika kama mchango wa mfanyakazi.
Kwa upande wake Afisa mafuatiliaji wa mfuko ofisi katika ofisi ya Songea (Compliance Officer), Mussa Adma alielezea mafao mbalimbali ambayo yapo chini ya NSSF kwa wanachama. Bw. Adam alifafanua kuwa kuna aina kuu mbili ya mafao yanayotolea na mfuko, ambayo ni mafao ya muda mrefu na mafao ya muda mfupi.
Alisema kuwa mafao ambayo yako chini ya mafao ya muda mrefu ni mafao ya pensheni ya uzeeni, mafao ya mkupuo maalum, pensheni ya ulemavu na pensheni ya urithi.
Katika mafao ya muda mfupi kuna mafao ya matibabu (SHIB), ambao hutolewa kwa wanachama na wategemezi wake ambao ni mume/mke na watoto wasiozidi wanne  wenye umri usiodizi miaka 18 au 21 ikiwa wanasoma mafao ya uzazi, mafao ya kuumia kazini na mafao ya msaada wa mazishi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...