Skip to main content

MAMIA YA WAKAZI WA IRINGA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAMZIKA DC CHANG'A


msigwa2_6544d.jpg
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) akiteta jambo na mmoja wa waombolezaji wa msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Moshi Chang'a wakati wa maziko katika makaburi ya Mtwivilla yaliopo Kihesa Manispaa ya Iringa mkoani Iringa leo.
mtoto_2_68c4b.jpg
Mwandishi wa habari wa www.fridaysimbaya.blog.com, Friday Simbaya (kushoto) akipata taarifa kutoka kwa mtoto wa mwisho wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, marehemu Moshi Chang'a, Hamis Moshi Chang'a wakati wa maziko katika makaburi ya Mtwivilla yaliopo Kihesa Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa leo.(Picha na Sagine Edward Majura)

mtoto_4_181f1.jpg
Mtoto mwingine wa marehemu Moshi Chang'a, Shabaan Mosji akifarijiwa na baadhi ya waombolezaji nyumbani kwa baba yake Kihesa kwa Mwachang'a baada ya maziko leo.
mtoto_8a82d.jpg
Mtoto wa mwisho wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Moshi Chang'a, Hamis Moshi Chang'a (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya waombolezaji makaburini leo.
rc_fdf6a.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Christine Ishengoma (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo wakifurahia jambo nyumbani kwa marehmu Moshi Chang'a  leo.
rpc_f8afc.jpg
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa (RPC), Kamnshina Msaidizi wa Polisi (ACP), Ramadhani Mungi (katikati) akifuatilia maziko kwa makini katika makaburi ya Mtwivilla Kihesa leo. RPC Mungi alikuwa ni mmoja ya viongozi wa polisi walioudhulia mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, marehemu Moshi Chang'a.
sheikh_kalambo_08bab.jpg
Sheikh wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Athuman Amani kutoka Msikiti wa Masijid N-aor akitoa mawaidha na shukurani kwa niaba ya waumini wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa baada ya mazishi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, marehemu Moshi Chang'a makaburini leo mchana.
sheikh_2b171.jpg
Sheikh wa Wilaya ya Iringa mjini, Issa Ngwele akiongoza dua wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Moshi Chang'a,ambaye ameacha watoto watano, watoto wakiume wa tatu na wawili wa kike.
umati_4f018.jpg
Umati wa waombolezaji makaburini.
wamzika_58da0.jpg
askofu_1351e.jpg
Afisa Utalii wa TANAPA katika Nyanda za juu Kusini, Risala Kibongo na Askofu  wa KKKT Iringa, Mdegella wakifurahia jambo nyumbani kwa marehemu Moshi Chang'a. 
chama_na_dini_a667e.jpg
Askofu Mdegella na Mwenyekiti wa Wilaya ya Iringa Mjini (CCM), Abeid Yusufu Kiponza. Askofu Mdegella ashikilia msimamo ule ule wa  serikali mbili, asema kamwe hatabadilisha msimamo wake.
dc_95206.jpg
gagag_e7f3d.jpg
IMG_4617_56962.png
Kaimu Katibu wa Mkoa CCM Iringa, Miraji Mtaturu (kushoto) akitoa salamu kwa niaba ya chama mkoa wa Iringa.
kandolo_0882b.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro wakibadilishana mawazo na baadhi ya waombolezaji nyumbani kwa marehemu Moshi Chang'a.
meya_e51e1.jpg
Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani mwamwindi (katikati) akitoa salamu.
morners_c8d04.jpg
Baadhi ya waombolezaji wakifuatilia maziko.
(PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA)
Na Friday Simbaya
Mamia ya wakazi wa mji wa Iringa wamzika aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, marehemu Moshi Chang’a katika makaburi ya Mtwivilla Manispaa ya Iringa mkoani Iringa leo mchana. 
Mkuu wa Wilaya Chang’a alifariki dunia Aprili 20, 2014 kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu. 
Shughuli ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu Chang’a kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ilifanyika jana mchana nyumbani kwake Mbagala, Kibonde Maji, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.  
Marehemu Chang’a amezikwa leo Kihesa, Manispaa ya Iringa ambapo Serikali imewasilishwa na Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia. 
Marehemu ameacha watoto watano, wa kike watatu na wa kiume wawili, Mungu alaze roho ya marehemu mahala pema. Amina.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...