Skip to main content

Ukawa wapata pigo


bunge 4c2f3

'Bunge Maalumu la Katiba, jana liliridhia azimio la kuzifanyia marekebisho kanuni zake saba bila kuwapo kwa wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao wamesusia Bunge hilo.

Marekebisho hayo ya kanuni yanaonekana kuwa pigo kubwa kwa wajumbe hao wa Ukawa kwa vile sasa hawatapewa tena fursa ya kufafanua maoni ya wachache badala yake watasoma tu.
Awali, Kanuni ya 33 ilikuwa ikitaka mwenyekiti wa kamati kutumia muda wa dakika 60 kusoma taarifa yake iliyokuwa ikijumuisha maoni ya wajumbe walio wengi na taarifa ya wale walio wachache.
Lakini kanuni hiyo sasa imefanyiwa marekebisho, ambapo mwenyekiti wa kamati atasoma tu taarifa ya walio wengi na maoni ya walio wachache yatasomwa na mmoja wa wajumbe wa walio wachache.
Kanuni hiyo ya 33(5) sasa itasomeka: "Maoni ya wajumbe walio wachache yatasomwa na mmoja wa wajumbe ambao hawakuunga mkono maoni ya wajumbe walio wengi kwa muda usiozidi dakika 30."
Akiwasilisha maelezo ya Kamati ya Maadili na Haki za Bunge, mjumbe wa kamati hiyo, Evod Mmanda, alisema kuwa hakutakuwa na nafasi tena ya mjumbe kutoka kundi la wachache kutoa mambo kichwani.
Mmanda aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Pandu Ameir Kificho, alisema maoni ya wachache yaligeuzwa kuwa maoni ya kisiasa na kubeba hoja za kishabiki za kisiasa. Alisema kuwa kutokana na marekebisho hayo, hakuna jambo litakalokuwa halijajadiliwa kwenye kamati, ambalo litaruhusiwa kusomwa na walio wachache ndani ya Bunge Maalumu la Katiba.
Kanuni nyingine zilizorekebishwa ni pamoja na ya 32, ambayo sasa inaruhusu mjumbe yeyote au kundi lolote la wajumbe kupendekeza sura mpya kwenye Rasimu ya Katiba.
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ina Sura 17.
Kanuni nyingine zilizorekebishwa ni 35, 41, 60, 62 na 82 pamoja na sehemu inayohusu orodha ya yaliyomo katika kanuni hizo za Bunge za mwaka 2014.
Akichangia hoja ya marekebisho hayo, mjumbe wa Bunge hilo, Anjelina Samike alisema kwamba wajumbe kutoka kundi la walio wachache walikuwa na maneno magumu na yasiyo na staha.
Kwa upande wake, Yusuph Singo alisema nafasi waliyokuwa wakipewa walio wachache, hawakuitumia kutoa ufafanuzi, badala yake waliitumia kujadili na kuibua mambo mapya.Baada ya kupitishwa kwa marekebisho hayo, Sitta alisema kanuni hizo zitaanza kutumika mara moja.
Wajumbe wanaotokana na Ukawa walisusa kuhudhuria vikao vya Bunge hilo wiki iliyopita kwa kile walichodai kupinga ukiukwaji wa kanuni na matumzi ya lugha ya matusi, kejeli na dhihaka.
CHANZO MWANANCHI

Tuma Maoni

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...