Skip to main content

‘Ushirikina’ Wakwamisha Mapambano ya Mimba kwa Wanafunzi Mbeya Vijijini


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usoha Njiapanda iliyopo Mbeya Vijijini.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usoha Njiapanda iliyopo Mbeya Vijijini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, , Willson Mwamunyila (katikati) akizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini kwake.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, , Willson Mwamunyila (katikati) akizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini kwake.
Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Usoha Njiapanda wakiwa katika mkutano na mwanahabari hizi.
Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Usoha Njiapanda wakiwa katika mkutano na mwanahabari hizi.
VITISHO na hofu ya vitendo vya ushirikina imebainika kuwa vikwanzo vya mapambano ya baadhi ya watu wanaowatia mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya.

Kauli hiyo ilitolewa juzi mjini hapa na baadhi ya wanakijiji kutoka katika baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela walipofanya mahojiano kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi alipotembelea vijiji hivyo. Akizungumza mkazi wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Maria Kolneri alisema baadhi ya wazazi hushindwa kuwawajibisha watu waliowatia mimba wanafunzi kwa kuhofia usalama wao kwani familia iliyotuhumiwa hujenga uhasama na familia ya mwanafunzi na hata kutoa vitisho.
Alisema katika kijiji hicho ni vigumu kwa familia ya mwanafunzi aliyetiwa mimba kufuatilia ili sheria ichukuwe mkondo kwani huwa kuna vitisho na vingine kutoka kwa majirani wa familia hizo. “…Hapa ukianza tu kumfuatilia mtu aliyefanya kosa kama hilo unasikia wanakijiji wanaanza kulalamika anataka kumfunga mwenzake sasa mtoto atakaye zaliwa atalelewa na nani…? Watakusema huku familia yenye kosa ikitoa vitisho hadi utaacha kufuatilia,” alisema. “Ukitaka kupata kesi (uhasama) hapa kijijini kwetu mfunge kijana aliyempa mimba mtoto wako…, kila mwanakijiji anayekujua atakuona hufai kwa madai kuwa umemwonea kijana uliyemshtaki,” alisema mama huyo.
Aidha aliongeza kuwa baadhi ya familia uhofia vitendo vya ushirikina (kulogwa) endapo utaendelea kufutilia kesi za mimba hivyo kukata tamaa, jambo ambalo kwa sasa kijijini hapo limekuwa la kawaida. Naye Nazareti Kibaga mkazi wa Kijiji cha Simambwe alisema kutokana na hali hiyo wananchi wamekuwa wagumu kufuatilia kesi za mimba jambo ambalo limefanya matukio hayo kuendelea licha ya changamoto zingine zinazochangia uwepo wake. “…Hali hii imefanya mimba ziendelee na hakuna kesi yoyote dhidi ya wanaowatia mimba wanafunzi…, wazazi hawawajibiki, wananchi hawawajibiki na viongozi nao hawawajibiki,” alisema Kibaga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Willson Mwamunyila alikiri uwepo wa matukio ya mimba kwa kiasi kikubwa kijijini hapo lakini alisema kikwazo katika kushughulikia matukio ya mimba ni uongozi kukosa ushirikiano kutoka kwa wazazi na mwanafunzi. “…Matatizo ya mimba yapo lakini wazazi na wanafunzi waliotiwa mimba hugoma kutoa ushirikiano kwa viongozi ili wahusika washughulikiwe kisheria.
Unakuta mtoto kapata mimba baada ya taarifa kukufikia unaenda kwa mzazi wa mwanafunzi kuomba ushirikiano lakini wazazi wengine wanakuzunguka wanazungumza na mwalimu kwenye shule husika na wanamalizana wenyewe,” alisema Willson Mwamunyila. (Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na TGNP)(FS)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...