Skip to main content

WAZIRI WA FEDHA: BAJETI YA MWAKA 2014/2015 NI SH19.6 TRILIONI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na  Waziri wa Fedha, Saada Mkuya kwenye mkutano wa wabunge ambapo waziri wa fedha aliwasilisha mapendekezo na mwelekeo wa bajeti ya serikali  kwa mwaka fedha 2014/15, Dar es Salaam jana. Picha na Salim Shao

Dar es Salaam. Serikali imetoa mwelekeo wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/15 kuwa ni Sh19.6 trilioni, ikilinganishwa na Sh18.2 za Bajeti iliyopita.
Vipaumbele vya Bajeti hiyo ni kuendeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulioanza mwaka 2011 na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao unajumuisha maeneo sita ya kitaifa ya kilimo, elimu, maji, utafutaji wa rasilimali fedha, nishati, uchukuzi na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara.
Katika kuhakikisha inakusanya fedha za kutosha, Serikali imeahidi kuunda kikosi kazi cha kufuatilia mapato yote yanayotoka halmashauri zote nchini ili kuondoa visingizio vilivyojitokeza wakati wa ufuatiliaji wa mapato.
Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya wakati akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti hiyo kwa kamati zote za Bunge, Dar es Salaam.
Alisema matumizi ya kawaida kwa mwaka ujao wa fedha yanalenga kufanikisha mambo 20 muhimu, yakiwamo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014, Uchaguzi Mkuu 2015, kukamilisha mchakato wa Katiba na nyongeza ya mishahara na kulipa kwa wakati.
Mkuya alisema makadirio ya matumizi ya maendeleo ni Sh7.7 trilioni sawa na asilimia 39 ya matumizi yote ya Serikali.
Kati ya fedha hizo, miradi ya maendeleo imetengewa Sh5.4 trilioni sawa na asilimia 27 na matumizi mengine ya maendeleo ni Sh2.2 trilioni.
Utegemezi
Mkuya alisema katika mwaka unaomalizika, Serikali ilipanga kukopa Dola 700 milioni za Marekani sawa na Sh1.1 trilioni na kati ya kiwango hicho, iliambulia mkopo wa Dola 259 milioni hivyo kuweka nakisi ya Dola441.
Alisema katika mwaka wa fedha 2014/2015, Serikali imekusudia kukopa Sh4.2 trilioni kutoka vyanzo vya mapato vya ndani na nje ili kuziba pengo la mapato.
Misaada na pato la taifa
Katika mwaka wa 2013/2014, Serikali ilipokea misaada ya Sh1.1 trilioni kutoka kwa washirika wa maendeleo ikiwa ni asilimia 50 ya ahadi ya Sh2.3 trilioni, hivyo kuweka nakisi ya Bajeti ya Sh1.2 trilioni. 
Akiwasilisha Rasimu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2014/2015, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema deni la Taifa limefikia Sh27.04 trilioni kutoka Sh24 trilioni na kufafanua kuwa ongezeko la deni hilo limetokana na mikopo mipya ya kibiashara na ya masharti nafuu.
Ukusanyaji mbovu wa mapato
Akizungumzia ukusanyaji wa kodi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kumekuwa na matatizo katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, hasa yasiyotokana na kodi.
“Tumepata changamoto na tunajiuliza kwa nini hatufikii malengo, lakini tunaamini kwamba tukijipanga vyema kwenye halmashauri zetu kwa kuzibana vyema, tutaweza kupiga hatua nyingine kutoka hapa tulipo,” alisema. (CHANZO:MWANANCHI)(FS)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...