Skip to main content

CCM YAIBOMOA NGOME YA CHADEMA

KADI_MPYA_2f8f6.jpg
KADI_7a59a.jpg
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akipokea kadi ya CHADEMA kutoka kwa Desius Nyoni (kushoto) aliyekuwa Afisa Habari Msaidizi Wilaya ya Mufindi katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana. 

MIRAJI_b2066.jpg
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya wa Mufindi, Komredi Miraji Mtaturu akitoa hotuba.

MTENGA_e6c14.jpg
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akihutubia
SHANGWE_95854.jpg
Wafuasi na wanachama wa CCM wakishangilwa ushindi wa chama hicho baada kuzoa wanachama 170 kutoka Chadema katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA

SHINA_594b5.jpg
AFISA_HABARI_16878.jpg
Alikuwa ni afisa habari wa CHADEMA Wilaya ya Mufindi, Rubeni Mwagala, akimwaga manyanga katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.
NA FRIDAY SIMBAYA, MUFINDI
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi kimeisambaratisha ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kufanikiwa kuvuna viongozi na wanachama 170 wa CHADEMA akiwamo Afisa Habari wa Wilaya hiyo, Rubeni Mwagala.
Viongozi na wanachama hao wa CHADEMA wakiongozwa na Rubeni Mwagala, ambaye alikuwa ni afisa habari wa CHADEMA Wilaya ya Mufindi, walitangaza rasmi kuachana na chama hicho katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa jana.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alizindua shina la wakeleketwa CCM Nyololo na baadaye aliwakabidhi kadi za uanachama wa wanachama wapya katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa kijiji hicho.
Viongozi wengine wa Chadema waliohamia CCM ni pamoja na afisa habari msaidizi wa wilaya ya mufindi, Desius Nyoni na Afisa habari muamasishaji wa wilaya hiyo Meja Mfilinge.
Wana CHADEMA hao waliohamia CCM walikiponda vikali chama hicho kimejaa ubabe, ukabila na kwa kufanya siasa za vurugu hapa nchini.
Kwa upande wake afisa habari huyo wa CHADEMA, Rubeni Mwagala aliwaomba radhi wananchi wa Nyololo kwa polisi kuwapiga mabomu tarehe 2 Septemba mwaka 2012 na kupelekea kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi katika Kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa akiwa kama afisa habari wa Chadema wilaya ya Mufindi ndiye aliyeratibu kufanyika mkutano na kupelekea mwandishi wa habari wa Chanel Ten Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC), Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Naye Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliwasihi wananchi waKijiji cha Nyololo na kwengineko wasibeze hatua ya maendeleo yaliyofanywa na chama tawala.
Alitoa mifano hiyo ya maendeleo katibu huyo alisema wakati nchi hii inapata uhuru kutoka kwa wakoloni nchi ilikuwa barabara za lami kilometa 300, lakini mpaka sasa kuna barabara za lami zenye urefu kilometa 17,800.
Alisema nchi wakati huo ilikuwa na vyuo vikuu vichache lakini leo hii ina jumla ya vyuo vikuu 34 na kuongeza kuwa hapo zamani kulikuwa na madakatari bingwa wachache lakini leo hii kuna madaktari bingwa 5200.
Aliwaasa pia wananchi kulinda amani iliyopo nchini kama mboni ya jicho na kuongeza kuwa ni heri kula dagaa kwenye nyumba yenye amani kuliko kula minofu ya sangara kwenye nyumba ya vita.
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi komradi Miraji Mtaturu alisema wakati umefika sasa wananchi wa Mufindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015, pigeni kura za hasira baina ya CHADEMA na kisha kuisambaratisha kabisa ngome hiyo kuwachagua viongozi wa kwa maendeleo yao.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...