Skip to main content

MAJALIWA MGENI RASMI SIKU YA WALIMU DUNIANI MANISPAA YA IRINGA





Na Friday Simbaya, Iringa
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya Iringa Manispaa, Fortunatafatuma Njalale amesema mgeni rasmi katika kilele cha siku ya waalimu duniani kiwilaya atakuwa Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi TAMISEMI, Kasimu Majaliwa (MB).

Alisema kuwa sherehe zinatanguliwa na juma la elimu siku ya walimu duniani Wilaya ya Iringa Manispaa kuanzia tarehe 29/09/2014 hadi 01/10/2014 ambapo itakuwa ni siku ya kilele kiwilaya katika Uwanja wa Samora, ili kujiandaa na sherehe hizo zitakazofanyika kitaifa mkoani Bukoba tarehe 5 mwezi Oktoba mwaka huu.
“Sisi wilaya na mikoa huwa tunafanya sherehe hizo siku ya walimu duniani kabla ya kilele kitaifa ili kuwapa na nafasi viongozi mbalimbali wa wilaya na mikoa kushiriki katika sherehe za kitaifa ukizingatia Bukoba ni mbali sana…,” alifafanua.
 Kila tarehe 5 mwezi wa kumi kila mwaka, huwa ni siku ya Walimu Duniani. Siku hii ya walimu duniani hutafakari walikotoka na changamoto wanazopata wakiwa kazini.
Aidha, katibu huyo alisema kuwa katika juma hilo la sherehe za siku ya walimu duniani kiwalaya chama hicho kitafanya shughuli mbalimbali pamoja na kuwa na mkutano wa uzinduzi wa ndani, ambapo mgeni rasmi alitarajia kuwa rais wa CWT Taifa, Gratian Mkoba lakini mgeni rasmi huyo kwa bahati mbaya amepata hudhuru.
Aliongeza kuwa kutokana na mabadiliko ya ratiba hiyo wamepanga kukutana na kiongozi huyo wa kitaifa baada ya sherehe hizo kumalizika kwa ajili ya kuongea na walimu Manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa shughuli zingine zitakazofanyika katika sherehe hizo ni pamoja na kuona watoto wagonjwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa, usafi wa soko katika soko kuu Manispaa ya Iringa, mashindano ya michezo ya riadha, mashindano ya mpira wa pete na miguu timu za walimu na timu za nje na hatimaye kufanya maandamano kuanzia Manispaa ya Iringa hadi katika Uwanja wa Samora kwa ajili ya kilele cha sherehe hizo ki wilaya hapo tarehe 01/10/2014.
Hata hivyo katibu huyo alitoa wito kwa walimu wote wa Wilaya ya Manispaa ya Iringa kujitokeza kwa wingi ili waweze kuonyesha vipaji mbalimbali pamoja kuonyesha ubunifu wao katika masomo mbalimbali.
Kauli mbiu ya maandhimisho mwaka huu; wekeza katika elimu kwa ajili ya maendeleo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...