Skip to main content

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA AFUNGUA PAZIA...!



Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa

PAZIA la kinyang’anyiro cha ubunge jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaelekea kufunguliwa baada ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu kuthibitisha kuwania nafasi hiyo. 

Akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulaman Kinana mkoani hapa, Msambatavangu ambaye pia ni diwani wa Kata ya Miyomboni mjini Iringa alisema; “nitagombea.”
Alitoa jibu hilo baada ya kuulizwa na wanahabari hao kama ana azma hiyo kufuatiwa kuwepo kwa tetesi zinazomuhusisha na kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kuwa na mchuano mkali ndani ya chama hicho.
Kama atatimiza azma yake hiyo, Msambatavangu atakuwa anaingia kwa mara ya pili katika kinyang’anyiro hicho ikikumbwa kwamba katika kura za maoni za chama hicho za mwaka 2010 zilizoshirikisha wagombea 12 alishika nafasi ya nne baada ya kujipatia kura 916, nyuma ya Frederick Mwakalebela aliyepata kura 3,897, Monica Mbega 2,989 na Dk Yahaya Msigwa aliyepata kura 1,217.
Wengine walioshiriki kinyanganyiro cha 2010 na kura zao kwenye mabano ni Fadhili Ngajilo (536), Addo Mwasongwe (383), Zuberi Mwachula (324), Benigus Mpete (242), Thomas Kimata (201), Chelestino Mofuga (192),  Dk Raphael Kalinga (169) na John Kiteve (136).
Katika kinyang’anyiro cha mwakani mbali na Msambatavangu aliyethibitisha kuwania nafasi hiyo wengine wanaotajwatajwa ni pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mahamudu Madenge ambaye hata hivyo amenukuliwa mara kadhaa akisema; “muda haujafika, hayo ni mambo ya mwakani kama tutakuwa hao, kazi tunayoendelea nayo sasa ni ya kuimarisha chama.”
Mbali na Madenge, makada wengine wanaotajwatajwa ndani ya chama hicho ni pamoja na Nuru Hepautwa anayefanya kazi zake zikiwemo biashara jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela.
Pamoja nao yupo pia Dk Yahaya Msigwa, Fadhili Ngajilo na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati ambaye amenukuliwa mara kadhaa akisema atajitosa katika jimbo la Iringa Mjini au Kilolo kama viti maalumu vitafutwa.
Katika mkutano wa hadhara alioufanya Januari 27, mwaka jana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Phillip Mangula atoa ruksa kwa wana CCM wanaotaka ubunge na udiwani katika majimbo na kata zinazoshikiliwa na wapinzani kuanza kupitapita ili kutafuta ushawishi.       
Wakati akitoa ruksa hiyo, Mangula aliuliza “…Iringa tulishindwaje jimbo hili, alitokea pepo gani, naomba mkemee pepo hao waliosababisha tushindwe ili 2015 turudishe  jimbo letu.”

Akizungumzia ukomo wa ruksa hiyo, Mangula alisema haihusu nafasi ya Rais na majimbo na kata zinazoongozwa na wana CCM.
“Nimeambiwa wapo walioanza kujenga makundi ndani ya chama kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao. Napenda kurudia tena ni marufuku kwa wanaCCM kuwabugudhi wanaCCM wenzao waliopo madarakani,” alisema.
Katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa, Mangula alisema wanaCCM wanaojipitisha kwenye maeneo yanayoongozwa na viongozi wa CCM, wataenguliwa hata kama watashinda kura za maoni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alisema kujipitisha katika maeneo wanayoyaongoza kunakibomoa chama hicho kwasababu ni chanzo kikubwa cha makundi.
“Mgogoro mkubwa ndani ya CCM ni makundi, makundi haya hujengwa kipindi cha kuelekea uchaguzi, hayana la maana zaidi ya kutubomoa. Hivi sasa nimeambiwa wapo walioanza kujenga makundi,” alisema.
Kinana na ujumbe wake wanatarajia kufanya ziara ya siku tatu mkoani Iringa ambayo pamoja na mambo mengi inalenga kukiimarisha chama hicho kwa kupokea na kuwaapisha wanachama wapya wakiwemo wanaotaka kujitoa kutoka vyama vya upinzani.
Ziara hiyo kwa mujibu wa Msambatavangu itaanzia wilayani Mufindi  Oktoba 6, mwaka huu na kuendelea katika wilaya ya Kilolo na Iringa Vijijini kabla ya kuhitimishwa Iringa Mjini. (BONGOLEAKS)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...