Skip to main content

NYALUSI:MAANDAMANO YA CHADEMA IRINGA YAKO PALEPALE...!

wakazi_1e654.jpg
mwt_2_f4391.jpg
Mwenyekti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Iringa Mjini, Frank Nyalusi akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya kitanzini leo.
mwt_d95b0.jpg

mkazi_91e43.jpg
Mkazi wa Kitanzani Claud Mahembe akiuliza swali la kutaka kupata ufafanuzi kweni bunge la katiba maalum halisitishwi kwa mwenyekiti wa Chadema Wilaya Iringa Frank Nyalusi wakati wa mkutano wa hadhara jioni leo.

Na Friday Simbaya, Iringa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Iringa Mjini limeshindwa kufanya maandamano ya amani kama ilivyotangazwa kwa kile kilichoelezwa na Mwenyekiti wake, Frank Nyalusi "tumepokea zuio kali kutoka jeshi la Polisi."

Akizungumza katika mkutano wadhara uliyofanyika Kata ya Kitanzaini mjinin Iringa, Nyalusi alisema wata fanya maandamano hayo Jumatatu wiki ijayo ikiwa ni kuitikia wito uliotangazwa na Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe wa kufanya maandamano ya amani yasio na ukomo yenye lengo la kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba.
Alisema pamoja na jeshi hilo kuwazuia kufanya maandamano jana hiyo hiyo waliruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wenye machinga wengi maarufu kama magari mabovu, Kitanzini.
Akieleza kushangazwa na maamuzi ya Polisi ya kuzuia maandamano yao, Nyalusi alisema maazimio yaliofikiwa katika mkutano huo nikufanya maandamano Jumatatu hata bila ya kibali cha polisi.
Wakati Chadema wakidai kudhibitiwa kufanya maandamano hayo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema jeshi hilo halijapokea barua yoyote kutoka katika chama hicho inayoonesha wameomba kufanya maandamano hayo.
Akitoa ufafanuzi huo kwa njia ya simu, Mungi alisema "nchi hii kama zilivyo nchi nyingine inaendeshwa kwa sheria, taratibu na kanuni."
Alisema watanzania bila kujali wanatoka kundi gani ni lazima wafanye mambo wanayotaka kufanya kwa kuzingatia sheria vinginevyo mkono wa sheria utawafukuzia.
Alisema mji wa Iringa upo shwari na kwamba jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kukabiliana na hali yoyote ile itakayoonekana inataka kuhatarisha amani.
Aliwataka wakazi wa Iringa kuendelea na shughuli zao kama kawaida na pale watakahisi au kusikia kuna mtu au kikundi chochote cha watu kinataka kufanya jambo linaloweza kuhatarisha usalama wao na wa mali zao, watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa Polisi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...