Skip to main content

VIJANA ZAIDI YA 3000 WAMALIZA MAFUNZO MAFINGA JKT

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148498854d27ed8e&attid=0.5&disp=inline&realattid=file5&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9BRHotx0LdPyXvG8i9awjW&sadet=1410159246518&sads=On4b_SgapWgEP6NvyubdZOgpJfo
Mgeni rasmi afande kanali John Julius Mbungo (mwenye miwani) ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa jeshi la kujenga taifa akipokea salamu na baadaye kukagua gwaride kwa, kumuakilisha mkuu wa jeshi la kujenga taifa kwenye sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya kuruti wa JKT kundi la miaka 50 ya muungano (kujitolea na mujibu wa sheria awamu ya kwanza 2014) katika kikosi cha 841 KJ Mafinga, mkoani Iringa.(PICHA NA FRIDAY SIMBAYA
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148498854d27ed8e&attid=0.3&disp=inline&realattid=file3&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9BRHotx0LdPyXvG8i9awjW&sadet=1410159353675&sads=mMv042QsbDPPxMKH2DDh0iVFZpU
Kijana wa kikundi cha kombati karate akionesha umahili wakunyanyua ndoo za maji kwa meno kwenye sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya kuruti wa JKT kundi la miaka 50 ya muungano (kujitolea na mujibu wa sheria awamu ya kwanza 2014) katika kikosi cha 841 KJ Mafinga, mkoani Iringa. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148498854d27ed8e&attid=0.4&disp=inline&realattid=file4&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9BRHotx0LdPyXvG8i9awjW&sadet=1410159473928&sads=wb0z5fdn97QC7aFs2rViBErY0hU
Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani kwenye sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya kuruti wa JKT kundi la miaka 50 ya muungano (kujitolea na mujibu wa sheria awamu ya kwanza 2014) katika kikosi cha
841 KJ Mafinga, mkoani Iringa leo. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=148498854d27ed8e&attid=0.6&disp=inline&realattid=file6&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9BRHotx0LdPyXvG8i9awjW&sadet=1410159583728&sads=O0AAn4_QozI57q9uzFo00UFPYuk
Kikundi cha kwata ya singe kikipata mbele ya mgeni rasmi na kutoa heshima kwa mwendo wa mchakamchaka kwenye sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya kuruti wa JKT kundi la miaka 50 ya muungano (kujitolea na mujibu wa sheria awamu ya kwanza 2014) katika kikosi cha 841 KJ Mafinga, mkoani Iringa  (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA

Na Friday Simbaya, Mufindi
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ametoa wito kwa vijana wanaohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi ambao ni vijana wa mujibu wa sheria na wa kujitolea kuzingatia kiapo cha utii walichoapa.
Akitoa wito huo kwa niaba mkuu wa jeshi la kujenga taifa, afande mgeni rasmi Kanali John Julius Mbungo, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa alisema kuwa vijana ni lazima wazingatie kiapo cha utii walichoapa mbele ya mgeni rasmi kwa Amiri Jeshi Mkuu wa
Majeshi na Usalama.
Alisema kuwa mafunzo waliopata ni kwa manufaa ya watanzania na sio kwa manufaa yao binafsi na pia wakumbuke kuweka miili yao ikiwa timamu kimazozi wakati wote.
Kanali Mbungo pia aliwaasa wahitimu hao kutojiingiza katika makundi yasiyofaa katika jamii na kutorubuniwa na makundi yanayotaka kuwagawa watanzania.
"Imarisheni mahusiano ya ushirikiano mliyojijengea mkiwa katika mafunzo haya. Mtumie ujuzi mliopata kuwafundisha na kuwaelekeza vijana ambao hawajapatia mafunzo ya JKT," alisema.
Aidha, wahitimu vijana wa mujibu wa sheria na wa kujitolea katika risala yao kwa afande mgeni rasmi walisema kuwa kulikuwepo na changamoto mbalimbali walizokumbana nazo wakati mafunzo kama vile; uhaba wa mavazi, upungufu wa magari katika mafunzo, uhaba wa maji na kucheleweshea posho pamoja na upungufu wa wakufunzi ukilinganisha na idadi ya wanafunzi.
Wahitimu haon waliiomba serikali kuongeza muda wa mafunzo kwa vijana wa mujibu wa sheria kutoka miezi mitatu sasa hadi kufikia miezi sita iliwaweze kuiva vizuri.
Hata hivyo, afande mgeni rasmi aliwaahidi kuwa changamoto zote zilizopo katika ngazi ya Jeshi la kujenga taifa zitashughulikiwa ipasavyo na kuongeza kuwa zingine ambazo zitakuwa juu ya uwezo wao watazipeleka ngazi ya juu.
"Natambua pia changamoto wanazozipata wakufunzi zikiwemo, upungufu wakufunzi ikilinganisha na idadi ya wanafunzi," alisema.
Sherehe ya kumaliza mafunzo ya awali ya kuruti wa JKT kundi la miaka 50 ya Muungano (kujitolea na mujibu wa sheria awamu ya kwanza 2014) katika kikosi cha 841 KJ Mafinga yalifanyika ambapo zaidi ya vijana 3,000 walihitimu mafunzo hayo jana (Ijumaa wiki) hii mjini Mafinga.
Sherehe hizo pia zilipambwa na burudani kutoka kwa vikundi vya vijana kwa kuonesha maonesho mbalimbali kama vile kwaya, kwata ya singe, kombati karati, ukakamavu, sarakasi, shairi na burudani toka brassband ya 841 KJ.
Jeshi la Kujenga Taifa ni moja kati ya taasisi muhimu mbayo ilianzishwa Julai 10, 1963, ikiwa maalumu kwa ajili ya kuwajengea vijana elimu ya kujitegemea, kuthamini utaifa wao, kujenga maadili ya kizalendo na kuheshimiana bila ubaguzi wa aina yoyote pamoja na kuwajengea ari ya kujitolea na namna ya kudumisha na kuimarisha amani na ulinzi wa taifa.
Vijana wengi, na hasa wasomi wa ngazi mbalimbali walikuwa walengwa katika dhana ya kuanzishwa kwa mafunzo ya kijeshi katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Kujenga Taifa nchini. Matokeo yake mazuri yalijidhihirisha katika maeneo mbalimbali ya kazi maofisini na hata katika kazi za mikono.
Nidhamu ya kufuata maadili mema inahitaji muda na uadilifu katika maandalizi ya hatua za awali kabisa kwa rika la vijana, na ndiyo maana mafunzo ya vijana kupitia Jeshi la Kujenga Taifa yalionekana kuwa mhimili mkubwa katika kuliandaa taifa kuwa na viongozi wazuri na waadilifu kwa miaka ijayo, dhamira ambayo inatakiwa iwe endelevu bila kikomo.
Kwa bahati mbaya sana, mafunzo hayo kwa vijana yalisitishwa mwaka 1994, lakini kwa sasa yamerejeshwa tena na vijana wanaomaliza kidato cha sita pamoja na baadhi ya vyuo vya elimu ya juu wanaendelea na mafunzo katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Kujenga Taifa nchini.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...