Skip to main content

Wafanyakazi wa Barabara Njia panda Kalenga walia hali ngumu ya maisha…!




 
Mlinzi wa kampuni hiyo (wa pili kutoka kulia) ambaye hakutaka kutaja jina lake akiongea na waandishi hivi karibuni ambapo alisema kuwa kampuni hiyo ina jumla ya walinzi watatu, lakini wana miezi miwili na siku 20 bila malipo.


 Mpishi Mkuu wa Kampuni ya ujenzi ya Canopies International, Agape Mgongola akiendelea na kazi yakuwapikia wafanyakazi wa kampuni hiyo bila malipo kwa miezi minne sasa. 

Na MARTHIAS KANALI, Iringa
Wakazi wa Kitongoji cha Msosa mkoani Iringa wameilalamikia kampuni ya Canopies International (T) Ltd kutoka Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambayo inajishugulisha na ujenzi wa barabara kutoka njia panda ya Kalenga kuelekea Tosamaganga kutokana na kushindwa kuwalipa fedha zao takribani miezi minne sasa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na THE SCOOP kijijini hapo wafanyakazi hao wamesema kuwa familia zao zimekuwa hazina msingi mzuri wa kimaisha kutokana na malimbikizo ya mshahara ambayo yawezekana wakalipwa ama wasilipwe kabisa, kwani mradi huo upo katika hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo.
Kwa upande wake mpishi mkuu Agape Mgongola ambaye ana miaka miwili tangu ameanza kufanya kazi na Kampuni hiyo tangu ilipoanza ujenzi wa barabara inayokwenda Kalenga hajawahi kupata usumbufu kama huu ambao anaupata kwa sasa. Agape alisema kuwa ni miezi miwili na wiki moja hajapatiwa malipo ya aina yoyote jambo ambalo ni la kustaabisha na kuathiri familia yake kiuchumi.
Aliongeza kuwa katika mkataba wake alipaswa kulipwa shilingi 35,000 kwa wiki, lakini hadi kufikia hivi sasa anadai jumla ya shilingi 315,000 kitendo ambacho kimekuwa tofauti na makubaliano ya malipo kabla ya kuanza kazi.
Akizungumzia adha wanayoipata kutokana na kutolipwa, mlinzi wa kampuni hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa kampuni hiyo ina jumla ya walinzi watatu, lakini wana miezi miwili na siku 20 bila malipo, hivyo kila mmoja anadai laki nne. "Sisi walinzi wa kampuni makubaliano yetu yalikuwa ni kwa mwezi, lakini hii ni miezi miwili na siku 20 sasa hakuna malipo hivi unadhani tunajikomboaje katika wimbi la umasikini kwa unyanyasaji na unyama tunaofanyiwa" alisema mlinzi huyo.
Mlinzi huyo alisema kuwa mwajiri wao amekuwa na dharau kwa watumishi hao, lakini hawana namna ya kujikwamua katika unyanyasaji, hivyo amaiomba serikali kuingilia kati na kutataua adha hiyo.
Wafanyakazi wa kampuni wanatoka sehemu tofauti tofauti hapa Tanzania ambapo wengine ni kutoka Dar es Salaam, Songea, Makambako na wengine wanatoka Iringa mjini. Wafanyakazi hao walisema kuwa unyanyasaji wanaofanyiwa na kampuni hiyo kuanzia kwenye malipo hadi wanapolala ni utumwa, kwani chumba kimoja wanalala watu zaidi ya 10.
THE SCOOP ilimtafuta Msimamizi wa malipo Ismail Joseph, ambapo majibu aliyatoa hayakuwa ya kuridhisha kwani alisema kuwa baadhi ya wafanyakazi hawatambui na wala hawezi kuwalipa.
Hata hivyo leo asubuhi nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama kiongozi wa Mradi huo wa barabara, ambaye alikiri kutowalipa wafanyakazi hao kama ambavyo wanalalamika.
Maungumzo kwa njia ya simu kati ya mwandishi na kiongozi huyo yalikuwa hivi; Mwandishi: Habari yako? Kiongozi: Nzuri natumai naongea na Mwandishi uliyefika jana ukafanya mahojiano na wafanyakazi wangu. Mwandishi: Ni kweli haujakosea, nikusaidie nini? Kiongozi: Taarifa uliyoipata jana kuhusu malipo ya wale watu ni kweli lakini hatujawalipa na hatutegemei kuwalipa hadi pale TANROADS. Kwa upande wake Meneja wa TANROADS Mkoa wa Iringa, Paulo Lyakurwa alisema kuwa kutolipwa ama kulipwa wafanyakazi hao sio jukumu la TANROADS, bali ni jukumu la kampuni hiyo. "Sisi tuliingia mkataba na Kampuni ya Canopies kwa hiyo, kampuni hiyo inapofanya kazi na vibarua ama wafanyakazi hawatuhusu sisi, tunapaswa kuhakikisha serikali imemlipa mkandarasi malipo yake kwa wakati japo kuna wakati malipo yao huchelewa, lakini sio sababu ya yeye kushindwa kuwalipa" alisema Lyakurwa.
Hata hivyo alisema kuwa atahakikisha anasimamia swala la malipo ili wafanyakazi hao waweze kulipwa kwa wakati.
 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...