Skip to main content

CHADEMA IRINGA YALITEGA JESHI LA POLISI

Mchungaji Peter Msigwa
Akiwa na Makamu Mwenyekiti Bavicha, Patrick Ole Sosopi
Sehemu ya watu waliojitokeza katika mkutano huo
Wakionesha ishara ya chama chao
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelitaka jeshi la Polisi kudhibiti misafara mirefu ya magari na pikipiki, na aina yoyote ya maandamano yatakayopangwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa wakati wa mapokezi ya katibu wake mkuu, Abdulahman Kinana.
Oktoba 6-11, mwaka huu Kinana atakayeambatana na Katibu Itikadi na Uenezi wa chama hicho Nnape Nauye anatarajia kufanya ziara ya kukijenga chama hicho na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika wilaya zote za mkoa wa Iringa.
Ombi hilo limekuja baada ya jana Jeshi la Polisi kuwadhibiti wafuasi wa chama hicho wa mjini Iringa kumlaki kwa maandamano ya magari na pikipiki, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) jimbo la Isimani, Patrick Ole Sosopi ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa Bavicha.
Sosopi aliyekuwa na Mchungaji Peter Msigwa wakitokea jijini Dar es Salaam kulikofanyika chaguzi mbalimbali za kitaifa za chama hicho, walipokelewa katika eneo la Igumbilo na viongozi wachache wa chama hicho baada ya Polisi kudaiwa kuwazuia wafuasi wao kuwapokea kwa misafara ya magari, bodaboda na maandamano.
“Tumetii maelekezo ya Polisi, vijana wetu wa bodaboda wamezuiwa kutupokea; ili haki itendekea tunataka Kinana na timu yake watakapoingia mjini Iringa, misafara yao isiwe na maandamano ya watu, pikipiki wala magari,” alisema Mchungaji Msigwa katika mkutano wao mkubwa uliofanyika katika kata ya Kihesa mjini Iringa.
Mchungaji Msigwa alisema watashangaa na kuchukua hatua endapo Polisi itairuhusu CCM kuwa na maandamano na misafara ya magari na pikipiki.
Naye Mwenyekiti wa Chadema wa Jimbo la Iringa Mjini, Frank Nyalusi alisema; “Kinana atakuwa mjini Iringa Oktoba 11, tukiona bodaboda wa CCM wako katika msafara wake nasi tutaingia barabarani tukiwa na wafuasi wetu madereva wa bodaboda na kufanya maandamano yasio na kibali.”
Makamu Mwenyekiti wa Bavicha Ole Sosopi alisema; “mimi ni kiongozi wa kitaifa, niliongea na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa kuhusu ujio wangu Iringa na mipango ya wafuasi wa Chadema kunipokea kwa shamrashamra. Nashangaa amekataa.”
Alisema kuyazuia maandamano ya Chadema na kuruhusu ya CCM kutadhihirisha jinsi Polisi wanavyokibeba chama hicho tawala.
Alisema wakati wakijiandaa kuchukua Dola wanataka kuona wanashindana katika uwanja sawa wa kisiasa kwahiyo hawatakubali kuona jashi la Polisi linaruhusu maandamano katika misafara ya Kinana wakati kwao linakataa. (Crediti to Bongeleaks)
Itaendelea……………………………..1

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...