Skip to main content

CHANJO YA SURUA-RUBELLA, MATENDE NA MABUSHA KUTOLEWA




Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inatarajia kufanya kampeni shirikishi ya ugonjwa wa Surua na Rubella kuanzia tarehe 18 hadi 24 oktoba, 2014.

Akizungumzia kampeni hiyo itakayofanyika nchini nzima jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Donan Mmbando amesema kuwa itawahusisha watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka 15.

Amesema kampeni hiyo itaambatana na utoaji wa matone ya Vitamini A, dawa za kutibu na kukinga magonjwa ya Minyoo, Usubi,Matende na Mabusha. 

Dkt. Mmbando amesema kuwa lengo na madhumuni ya kampeni hiyo ni kudhibiti milipuko ya magonjwa ya Surua na Rubella ili kupunguza vifo na madhara yanayosababishwa na magonjwa hayo.

“Katika kampeni hii tutatoa dawa za kutibu na kukinga magonjwa ya Minyoo, Usubi, Matende na Mabusha katika mikoa 16 yenye maambukizi makubwa ya magonjwa haya”, Amesisitiza Dkt. Mmbando.

Amefafanua kuwa chanjo ya Surua na Rubella itatoa fursa ya kutoa kinga kwa watoto wengi zaidi ambao hawakupata chanjo hiyo utotoni katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya magonjwa hayo ambayo ni Mtwara, Lindi, Tanga , Dar  es salaam,Morogoro, Pwani, Tabora, Manyara, Iringa, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Singida, Dodoma na Njombe.

Akitoa ufafanuzi kuhusu chanjo hizo amesema kuwa chanjo ya Surua na Rubella itatolewa kwa watoto wenye umri wa miezi 9 hadi chini ya miaka 15, matone ya vitamin A kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi chini ya miaka 5.

Nyingine ni dawa za minyoo (Mebendazole) zitakazotolewa kwa watoto wenye umri wa miezi 12 hadi chini ya miaka 5 nchi nzima na dawa za kutibu na kukinga minyoo (Albendazole) Usubi, Matende na mabusha au Ngirimaji kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 5 na kuendelea katika mikoa 16 iliyobainishwa.

Kwa upande wake Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  Dkt. Dafrosa Lyimo ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanawapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili waweze kupata chanjo  hiyo.

Pia ametoa wito kwa mama wajawazito kuhakikisha kuwa wanapata chanjo ya Surua-Rubella ili kuwakinga watoto wao dhidi ya matatizo ya Moyo, mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati na mtindio wa ubongo yanayotokana na ugonjwa huo.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...