Skip to main content

Chibuku Super yadhamini Uhuru Marathon 2014

 
 Meneja mauzo na usambazaji wa Darbrew Fred Kazindogo (kulia)
 
Na Mwandishi Wetu
 
KAMPUNI ya Bia za asili ya Darbrew (TBL) kupitia bia yake ya asili ya Chibuku super imetangaza kudhamini mashindano ya mbio ndefu za Uhuru ‘Uhuru Marathon’ kwa kiasi cha Sh.  milioni 6.
 
Akitangaza udhamini huo jana jijini Dar es Salaam, Meneja mauzo na usambazaji wa Darbrew Fred Kazindogo, alisema, wameona ni vyema kudhamini mbio hizo kwa sababu zina lengo la kuimarisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
 
Alisema huu ni mwaka wa pili kudhamini mbio hizo ambapo mwaka jana kampuni hiyo ilitoa kiasi cha milioni 5 na zilifanyika kwa mafanikio.
 
Alisema kuwa baada ya kuona malengo yametimia , Darbrew iliamua kuendelea kudhamini mbio hizo zinazoshirikisha wanariadha kutoka sehemu mbalimbali ndani ya nje ya nchi.
 
“Baada ya mwaka jana mbio hizi kufanyika kwa mafanikio makubwa, mwaka huu Kinywaji chibuku super kimeongeza udhamini wake kwa asilimia 15% ambazo ni ongezeko la milioni 1,’’ alisema kazindogo.
 
Ukweli ni kwamba taifa lolote duniani linapigania kuwa na uchumi imara na pasipokuwa na amani hakuna uchumi utakaoweza kukua, hivyo Darbrew kama kampuni inayotengeza bidhaa za hapa nyumbani imeona ni muhimu kuungana na Watanzania wenzetu wote kuhakikisha kuwa mbio hizi zinafanyika katika hali ya mafanikio makubwa na kuwa za kufana zaidi.
 
Aliongeza kwa kuyataka makampuni mengine ya ndani na nje ya nchi kujitokeza na pia kuendelea kutoa chochote walichonacho ili kufanikisha mbio hizi zenye kubeba dhima ya Taifa letu lakini pia wajitokeze kwa wingi kushiriki mbio hizi.
 
Naye mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck, aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo ambazo zina nia kubwa ya kutukumbukusha wajibu wetu wa kutunza na kulinda amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.
 
Alisema zawadi kwa mshindi wa kwanza inatarajiwa kuwa Sh. 2,500,000 kwa wakimbiaji wa kilomita 21 hii ni kwa upande wa wanawake na wanaume.
 
Mshindi wa pili kwa mbio hizo iwe kwa upande wa wanawake au wanaume kwa kilomita 21 au ataondoka na Sh 1.500,000 wa tatu Sh 1,000,000 wanne Sh 500,000 watano apata Sh 250,000 na wa sita hadi kumi sh 100,000 kila mmoja.
 
Pia mwaka huu kutakuwa na zawadi za ngao za heshima kwa shule za msingi na sekondari zitakazoshiriki mbio za hizo ili kutambua ushiriki wao na tayari shule 25 zimethibitisha kushiriki mbio kwa mwaka huu.
 
Mbio hizi zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam hapo Desemba 7, mwaka huu ambapo zitaanzia na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders club.
 
Mbio hizi zipo chini ya ulezi wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwa mara nyingine tena tunatarajia Mh Rais Jakaya Kikwete kushiriki mbio hizi,
 
Mbio hizo zimegawanywa katika makundi makuu matatu ambayo ni kilomita 3 kwa ajili ya viongozi, kilomita 5 kwa watu wote na kilomita 21  ambazo ni maalum kwa wakimbiaji nguli.
 
Wadhamini wengine wa mbio hizo ni pamoja na Michuzi Media Group, Jambo Leo, Mwananchi Communication Limited, CXS Africa, Kitwe General Traders, Faza Kidevu Blog, Habari Mseto Blog, Blog ya Wananchi,TBC 1,TBC Taifa,Redio Uhuru,Clouds fm,Tindwa medical service.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...