Skip to main content

CWT NJOMBE YATAKA SERIKALI ISITISHE BIASHARA HURIA YA VITABU VYA KIADA


Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya Njombe kimeitaka serikali kusitisha biashara huria ya vitabu vya kiada kwa kile walichoeleza kwamba vinakinza na kuwapa ugumu katika ufundishaji.
Ombi hilo lilitolewa hivi karibuni wakati chama hicho kikiadhimisha siku ya walimu iliyofanyika mjini Makambako, wilayani humo.
“Kama ikishindwa kusitisha, tunashauri kabla vitabu hivyo havijaingizwa sokoni, serikali ifanye utaratibu wa kubihariri na kuvigonga mihuri maalumu ili kuwahakikishia walimu kwamba vimethibitishwa,” alisema Katibu wa CWT Njombe, Salama Lupenza.  
Aidha chama hicho kimeita serikali kufanya tafiti za kutosha katika miradi yake ukiwemo mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) unaolalamikiwa kuwazidishia mzigo wa uwajibikaji bila nyongeza ya marupurupu.

Lupenza alisema pamoja na mpango huo kuanza kuongeza tija katika sekta mbalimbali za kimaendeleo, hali ya walimu imeendelea kuwa vile vile.
“Tunasikitishwa sana, pamoja na mafanikio ya BRN, hakuna chochote kinachofanywa na serikali kuboresha maslai ya mwalimu,” alisema.
Kwasababu serikali haizifanyii kazi kwa wakati kero mbalimbali zinazowasibu, Lupenza alisema katika maeneo mbalimbali nchini walimu wanapoteza hali ya kuipenda kazi hiyo na kuifanya kwa nguvu zao zote jambo linaloweza kuhatarisha zaidi maendeleo ya sekta hiyo.
“Kwa upande wa sekta yetu hii ya elimu, BRN inaonekana kumjali zaidi mwanafunzi lakini inamsahau mwalimu mwenye wajibu mkubwa wa kumuwezesha mwanafunzi kufikia mafanikio yake,” alisema.
Alisema tofauti na miaka ya nyuma ambapo kazi ya ualimu ilikuwa na hadhi kubwa mbele ya jamii, hivisasa hali hiyo haipo tena kwani ualimu imekuwa ni kazi inayodharauliwa na wengi. (bongoleaks)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...