Skip to main content

Dkt Slaa: Uzembe wa wanachadema ndio ushindi wa CCM

Na Mathias Canal,Iringa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza mikutano yake ya nchi nzima kama ilivyotangazwa na katibu mkuu wa chama hicho Dkt Wilbroad Slaa, hivi karibuni alipozungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.


Chadema kimeridhia kufanya mikutano nchi nzima ambapo katika mkoa wa Iringa mkutano huo ulianza jana katika viwanja vya Mlandege kwa kuhutubiwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Prof Abdalla Safari.

Akizungumza na mamia ya watu waliojitokeza katika mkutano huo ambao imeelezwa kuwa haujawahi kutokea mkutano kuwa na wimbi la watu kama hao, amesema kuwa ukombozi wa nchi ya Tanzania umetokana na damu ya watanzania hivyo hakukuwa na sababu ya watanzania kuishi maisha ya umasikini kama ilivyo kwa nchi kama hii yenye rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na misitu, madini na ardhi ya kutosha.

Safari alisema kuwa wananchi wa Botswana wanafaidika na madini ya nchi yao kwa serikali kukusanya 70% ya madini huku nchi kama Tanzania ikichukua 5% ya madini, hivyo ni dhahiri kuwa Uwezo duni wa kufikiri kwa viongozi wa Tanzania ndio sababu ya umasikini wa Watanzania na utajiri wa wananchi wachache (Mafisadi).

"Pia nawaahidi kwamba UKAWA tumeridhia kusimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi kuanzia ngazi ya serikali za mtaa hadi Taifa, lakini kubwa zaidi tunataraji kwenda mahakamani kuzuia mchakato wa katiba kukusanya maoni ya wananchi" alisema Safari.

Hata hivyo Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt Wilbroad Slaa amesema kuwa kuna daftari la mkazi linapita mtaani hivyo wananchi wanapaswa kujiandikisha kwa wingi ili wawe na uwezo wa kupiga kura sambamba na kujitokeza kuwania nafasi za uongozi wa serikali za mitaa.

"Mnapaswa kutambua kuwa siku 21 kabla ya kupiga kura ni muda wa kujiandikisha hivyo kila mmoja ajiandikishe na kuhamasisha wengine, nachukua nafasi hii kuwakumbusha kuwa uzembe wa wanachadema ndio ushindi wa CCM" alisema Slaa.

Slaa alisema kuwa CCM imeshindwa kutoa elimu bure kwa watanzania kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu tangu waingie madarakani hivyo wasitegemee kufanikiwa kwa kipindi kifupi kilichosalia.

Naye mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mch Peter Msigwa alijibu mapigo ya Katibu mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana alipozuru Mkoani Iringa hivi karibuni, alisema katibu huyo alitumia muda mwingi katika mkutano wake kumzungumzia badala ya kuzungumzia maendeleo ya nchi.

"Nilishinda kwa ushindi mnono mwaka 2010 kwenye uchaguzi mkuu hivyo nawaomba msikubali kupotoshwa na propaganda ya kwamba nilishinda baada ya CCM kujichanganya, tuna mambo mengi ya kuzungumza lakini tutaendelea kuonana mara kwa mara kwani muda wetu hautoshi, wapo waliosema mimi na Chiku Abwao tuna ugomvi hivyo ni rahisi kukomboa Jimbo la Iringa Mjini, hilo lisahaulike naamini mmemsikia wenyewe Chiku alichokisema".

Msigwa alisema kuwa kuhusu mfuko wa jimbo ameanza kupita kila Kata ili kutoa ufafanuzi kwa kina kwa kile kilichofanyika hatimaye watanzania kutopotoshwa na baadhi ya wanasiasa.

Kwa upande wake Salumu Mwalimu ambaye ni Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zanzibar amesema kuwa, Chadema kinaamini katika vijana ndio maana wengi wao ni viongozi na ufanisi wa hoja unaonekana.

Mwalimu alitumia nafasi hiyo pia kumuomba ruhusa Katibu mkuu wa chama hicho ili kurejea tena mkoani Iringa kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha na kujitokeza katika kuwania nafasi za serikali za mtaa.

Viongozi wengine waliohudhuria katika mkutano huo ni pamoja na Patrick Ole Sosopi Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa sambamba na Chiku Abwao Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...