Skip to main content

JESHI LA MKOANI IRINGA LINAMSHIKILIA NGAGA KWA MAUAJI YA RAFIKI YAKE



Na Friday Simbaya, Iringa
Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Gwerino Ngaga (70) mkazi wa Mbigili kwa kosa la kumpiga risasi  kifuani Thadei Mbugu(40) mkazi wa Mbigili  na kusababishia kifo chake papo hapo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi akielezea tukio hilo la kinyama kwa waandishi wa habari ofisini kwakw leo alisema kuwa limetokea Oktoba 9 majira ya saa moja za jioni  katika kijiji chaMbigili kata ya Lugalo tarafa ya mazombe wilaya ya kilolo mkoani hapa.

Kamanda Mungi alisema kuwa awali kabla ya tukio marehemu pamoja na mtuhumiwa wakiwa na wakezao walikuwa wakinywa pombe  za kienyeji katika kilabu kinachoendeshwa na mke wa Gwerino.

Mungi alisema kuwa sababu kubwa ya  mtuhimiwa kumpiga risasi marehemu Thadei lilitokea mara baada ya mke wa mtuhumiwa kumuomba pesa marehemu mbele ya mkwewe na mumewe kitendo kile kilimuudhi mtushtakiwa  na  kuamua kuenda nyumbani kuchukua bunduki aina ya shortgun na kumpiga  kifuani hali iliyopelekea kupoteza maisha.  



‘’Hawa jamaa walikuwa wote na wake zao wakipata kinywaji sasa wakati wanakunywa huyu mke wa mtuhumiwa alimuomba marehemu ampe hela ya  kutumia na mke wa  wa marehemu aliposikia mumewe akiombwa hela alifoka kwa nguvu kwa kulaani kitendo cha mumewe kumhonga mke wa mtu hela tena kilabuni huku angali akiwa na mumewe’’



“Sasa mume wa yule mke aliposikia mkewe anapewa hela na marehemu alimuuliza kisa cha kumdhalilisha kwa kumpa mkewe hela mbele yake ndipo marehemu akamjibu kwa dharau kuwa amezeeka na hivyo hana hela hivyo anamsaadia kumlea kitendo kilichomuudhi mstakiwa na kumlipua kwa bunduki yake,”  alisema Mungi.



Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi wa karibu ili kubaini nini chanzo hasa kilichosababisha mtuhumiwa kuchukua bunduki na kumpiga mwenzie kwani hapo awali kulikuwa hakuna ugomvi wowote na wote walikuwa ni majirani wanaokaa mtaa moja .

Mungi alieleza kuwa  baada ya kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa bunduki hiyo  aina ya shotgun iliyotumika katika mauaji hayo  inamilikiwa kihalali na Gwarino Ngaga mkazi wa Mbigili.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...