Skip to main content

KINANA AKUNWA NA UTENDAJI KAZI WA MBUNGE WA KALENGA

Katibu  mkuu  wa CCM Bw kinana  kushoto  akishiriki kuvua  samaki  Kalenga na  mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu 

 Kinana  akitazama  bwawa la  samaki na kuvua  samaki
Chifu  wa  wahehe   wa pili  kulia  akiwa na wasaidizi  wake  huku  kiti cha kinana  kikiwa  tupu 

Mkutano wa  Kinana  Kalenga 

Mwenuyekiti wa Halmashauri ya  wilaya ya  Iringa Stivin Mhapa  akieleza  utekelezaji wa ilani ya CCM mbele ya katibu mkuu wa CCM Bw Kinana 

Wanahabari  wakiongozwa na mhariri wa habari gazeti la Jamboleo Said Mwishehe  kushoto kutazama  fuvu la  chifu Mkwawa baada ya kutembelea makumbusho hayo jana 

Wanahabari  waliopo katika  msafara wa Kinana  wakitazama   fuvu la chifu Mkwawa 

Kinana  akiwa ameshika  bunduki ambayo chifu Mkwawa alikuwa akiitumia 

Chifu  wa  wahehe mrithi wa Mkwawa Bw Abdu Mkwawa akitoa maelekezo kwa katibu mkuu wa CCM Bw  Kinana mbele ya  fuvu  la Chifu  Mkwawa 

Kikundi  cha  mamalishe  ambao  walikuwa  Chadema  waliojiunga na CCM mbele ya  kinana 

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya  Iringa  vijijini  Delophina Mtafilalo  akimkabidhi kinana  kikapu  cha asili .

 KATIBU  mkuu  wa  chama  cha mapinduzi (CCM) Taifa , Abdulrahman Kinana  amesifu  utendaji  kazi wa mbunge wa  jimbo la Kalenga  Bw Godfrey Mgimwa  kuwa amekuwa ni mfano  wa kuingwa  kutokana na kuendelea  kuwa karibu  zaidi na  wapiga  kura  wake.


Kinana  akisaidia  kupulizia dawa nyanya katika kijiji  cha Kalenga  wakati wa ziara  yake 
" Kijana  Godfrey Mgimwa ni  hodari  sana kwani  ameendelea kufanya kazi  kwa  kujituma  zaidi kama alivyokuwa marehemu babake ......kweli  kijana   huyo amenifurahisha  sana kwani kipindi  hiki anachoongoza  si  cha kwake ni kipindi  cha marehemu babake ila  yeye ameendelea  kujitolea  zaidi na  kufanya kama alivyokuwa akifanya  babake  .....hivyo nampongeza sana   mbunge  wenu  huyo Godfrey Mgimwa "

Akizungumza katika mkutano wa hadhara  uliofanyika   jana

katika kijiji   cha Kalenga  alisema  kuwa mbunge  huyo ameiga  tabia ya  marehemu  babake kwa  kuendelea  kuwatumikia  wapiga  kura kwa unyenyekevu mwingi na  uwajibikaji wa hali ya  juu jambo  ambalo kwake  binafasi na  chama ni  njema  zaidi.

Kwani  alisema  kuwa  amekuwa akifuatilia katika  vyombo  mbali mbali vya habari  toka  alipochaguliwa na  kuona  jinsi  ambavyop mbunge  Mgimwa  anavyoendelea  kuwa karibu  zaidi na  wapiga  kura  wake kwa kila juma  kufika  jimboni  kuhamasisha na  kuchangia maendeleo ya  wana kalenga.

Kinana  alisema  marehemu  Dr  Wilaim Mgimwa  wakati wa uhai  wake  hakuwa na makuu na mtu  ila  alikuwa akipenda  kumsaidia  kila  mmoja  na wakati  wote  alikuwa ni kiongozi msikivu na mpre zaidi  mfano  ambao ameuiga  mwanae Godfrey Mgimwa ambae amekuwa  na  tabia  njema ndani  ya  chama na kwa  wapiga  kura  wake.

Hata  hivyo  alisema  kuwa ndoto ya  wana Kalenga  ni  kuendelea  kuona  wanapata  maisha  bora kwa  upande  wa wakulima  kusaidia  kuboreshewa  kilimo  chao kwa  kupata  pembejeo  ambazo ni  hitaji lao kazi ambayo Mgimwa anaiweza  kwa  kushirikiana na serikali ya  wilaya na mkoa.

Kuhusu miradi  mikubwa ya kimaendeleo  inayoendelea katika  jimbo  hilo Kinana  alisema kwa sasa  ipo miradi ya  umeme  kwa maeneo ambayo  hayajapata  kuwa na  umeme na kuwa umeme  huo ni  wa gharama  nafuu na  kudai kuwa  zote  hizo ni jitihada za  mbunge  huyo.

Pia   Kinana  alitaka  wananchi  viongozi wa  serikali  katika  mkoa  wa Iringa na  wilaya  hiyo kusaidia kuboresha maisha  ya  wananchi  hao  kwa kusaidiana na mbunge  Mgimwa  na  kuwa CCM isingependa  kuona  wananchi  wanaendelea  kuwa nyuma  kuteseka na kero mbali mbali  zinazowakabili . (MZEE WA MATUKIO DAIMA)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...